Skip to main content

DOSARI YAJITOKEZA KURA ZA MAONI UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI, MGOMBEA ATAKA MCHAKATO USITISHWE


frank Kibiki ambaye pia ni Mwanahabari wa Magazeti ya Uhuru na
Mzalendo wa mkoani 




frank Kibiki akionyesha walivyo kosea jina lake. 



na mwandishi wetu,iringa

WAKATI kura za maoni za kutafuta wagombea ubunge katika majimbo yote nchini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) zimekipigwa jana, mmoja kati ya wagombea 13 wanaotafuta nafasi hiyo Jimbo la Iringa Mjini, Frank Kibiki anataka zoezi hilo jimboni humo libatilishwe.

Wagombea wengine ni pamoja na Dk Augustino Maiga, Dk Yahaya Msigwa, Frederick Mwakalebela, Nuru Hepautwa, Michael Mlowe, Aidan Kiponda, Addo Mwasongwe, Jesca Msambatavangu, Mahamudu Mgimwa, Peter Mwanilwa na Fales Kibasa.

Akizungumza na wanahabari hii leo, Kibiki ambaye pia ni Mwanahabari wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa mkoani hapa alisema kura hizo zinapoteza uhalali kwasababu jina lake limekosewa.

“Mimi aitwa Frank John Kibiki, lakini kwenye karatasi ya kupigia kura ameandikwa mgombea mpya aliyetajwa kwa jina la Frank John Kibiri,” alisema.

Alisema kwa kuwa Frank Kibiki na Frank Kibiri ni watu wawili tofauti, hawezi kukubali kutumia jina la Kibiri ili kuhalalisha mchakato huo na endapo atafanya hivyo wagombea wenzake wanaweza kukata rufani kupinga matokeo hayo.

Kibiki alisema ameandika barua ya malalamiko yake kwa uongozi wa CCM wa Manispaa  huku kopi ya malalamiko hayo yanayotaka uchaguzi huo ufanyike upya baada karatasi ya kupigia kura kusahihishwa akiipeleka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.

Akikiri kupokea barua ya mlalamikaji huyo na dosari iliyojitokeza kwenye karatasi hizo za kupigia kura, Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi alisema; “suala hili tulikubaliana na mgomea huyo tulimalize kwa kusahihisha kwa peni jina hilo.

Baada ya kuifanya kazi hiyo kabla ya zoezi lenyewe la upigaji kura kuanza, zoezi limeendelea kama kawaida.”

Taarifa ya Mwampashi imepingwa na Kibiki mwenyewe aliyesema katika vituo 81 kati ya 90 vya upigaji kura alivyotembelea ni kituo kimoja tu cha Umati alichokuta jina lake limerekebishwa katika karatasi hizo.

Huku akiahidi kuishtaki kampuni iliyopewa kazi ya kuchapisha karatasi hizo kwa nkukosea jina lake, Kibiki alisema; “katika hili sitanyamaza, nitakuwa sauti ya yoyote aliyewahi kuonewa ndani ya chama vinginevyo nitalazimika kusubiri miaka mitano ijayo ili nishriki kwenye mchakato mwingine wa haki.” Alisema.

Wakati huo Katibu wa CCM wa Manispaa hiyo amezungumzia idadi ya wana CCM waliojitokeza katika mchakato huo wa kura za maoni kuwa ni ndogo ikilinganishwa  matarajio yao ya kushirikisha wanachama zaidi ya 18,000. 


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...