Skip to main content

PSPF WATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA LIGI YA MADEREVA WA BODABODA




Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya G Unity Fc kwa ajili ya mchezo wa fainali uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B katika kata ya Kipunguni manispaa ya Ilala jijini Dar. Ambapo timu ya G Unity FC waliibuka washindi baada ya kuichapa timu ya Sukuma Land Fc bao 5 kwa 2.



Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya Sukuma Land FC wakati wa mchezo wa fainali wa kombe la Madereva bodaboda wa kata ya Kipunguni.Wa pili kushoto ni ASP Mbunja Matibu kutoka Traffic Makao Makuu.


Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akitoa somo kwa madereva bodaboda kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari(PSS) waliofika katika mchezo wa fainali katika uwanja wa Kipunguni B






Mmoja wa Madereva Bodaboda akiendelea kupewa faida za mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) kutoka kwa Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto)


Mmoja wa madereva wa Bodaboda akijisajili kwenye mfuko wa (PSPF) kupitia (PSS) kwa ajili ya kuendelea kupata huduma zilizobora na zenye uhakika kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy 





Mmoja wa madereva wa Bodaboda akijiunga kwenye mfuko wa (PSPF) kupitia (PSS) ambapo kila mtu anaweza kujiwekea akiba kupitia kwenye mfuko huo wa hiari wakati wa mchezo wa fainali.


Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akiwasajili madereva wa Bodaboda kwenye mfiko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) wakati wa mchezo wa fainali wa Madereva bodaboda ambapo G Unity aliibuka mshindi kwa kumchapa Sukuma Land bao 5-2








Vijana waliofika katika mchezo wa fainali wakisoma vipeperushi vya mfuko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ambapo mfuko huo ulidhamini ligi hiyo iliyoendeshwa kwa wiki nzima






Mmoja wa Madereva Bodaboda akisoma maelekezo ya jinsi ya kutuma pesa kwenye akaunti kwenye mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) mara baada ya kupatiwa kitambulisho cha uanachama wa mfuko wa PSPF.


Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akimjazia fomu ya mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) mama aliyekuja kushabikia timu yake wakati wa fainali ya Kombe la Madereva bodaboda





Maafisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,waratibu wa michezo hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Timu ya Sukuma Land ambapo katika mchezo huo timu hiyo iliibuka mshindi wa pili baada ya kufungwa na timu ya G Unity Fc kwa mambao 5-2.




Maafisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa michezo hiyo pamoja na Timu ya G Unity Fc walioibuka washindi wa wa kwanza baada ya kufunga timu ya Sukuma Land Fc mabao 5 -2, mchezo huo uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B



Mchezaji wa Timu ya Sukuma Land Fc akiwatoka mabeki wa G Unity Fc ambapo katika mchezo huo timu ya G Unity Fc iliibuka mchindi wa mashindano hayo





Ilikuwa ni burudani katika mchezo wa fainali kati ya Timu ya G Unity Fc na Sukuma Land Fc



Gori kipa wa timu ya G Unity FC akijifunga gori wakati wa mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanhja wa Kipunguni B



Wachezaji wa Timu ya G Unity Fc wakishangilia baada ya kupata bao wakati wa mchezo wa fainali






Mbwembwe za mashabiki katika fainali hizo



Hizi ndizo zawadi zilizotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa mshindi wa kwanza mpaka wa nne katika mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda wa kata ya Kipunguni amabapo mshindiwa kwanza aliondoka na Mbuzi wawili na seti moja ya jezi, mshindi wa pili aliondoka na mbuzi mmoja na seti moja ya jezi, mshindi wa tatu aliondoka na seti moja ya jezi na mshindi wa nne aliodoka na mpira mmoja.



Mkurugenzi mtendaji wa kata
ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika mchezo wa
fainali akikabidhi mpira kwa kapteni wa timu ya Kilimani Fc walioibuka washindi
wa wa nne katika mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya
Kipunguni. Wa kwanza kushoto ni Afisa
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma.



Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde akiwakabidhi zawadi ya seti ya jezi timu ya Loliondo Fc baada ya kuibuka mshindi wa Tatu katika mashindano hayo.



Kapteni wa timu ya Sikuma Land Fc akipokea seti ya jezi mmoja na Mbuzi mmoja baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali hiyo. Wa kwanza kushoto ni ASP Mbunja Matibu kutoka Traffic Makao Makuu, wa pili kushoto ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy



Washindi wa mashindano ya mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya Kipunguni wakisalimiana mgeni rasimi wakati wa kukabidhiwa zawadi zao



Mkurugenzi mtendaji wa kata
ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde akikabidhi seti ya jezi na mbuzi wawili
wa kapteni wa timu ya G Unity Fc ambao waliibuka washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya
Kipunguni baada ya kuichakaza timu ya Sukuma Land Fc bao 5-2














MAshabiki wakiendelea kufuatia kinachijiri uwanjani


Mashindano ya ligi wa mpira wa miguu kwa madereva bodaboda yahitimishwa na wadhamini wa mashindano hayo ambao ni mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kuweza kuwasajiri wachezaji kutoka mfuko wahiari wa PSS. 

Ligi hiyo iliyodumu ndani ya siku saba (7) ambapo alikuwa akitafutwa mshindi atakayeweza kuwa balozi mzuri wa mfuko wa pensheni wa PSPF yamemalizika kwa timu 32 kumenyana vikali na timu ya G Unity kuibuka kinara ambapo timu hiyo ndiyo iliyotawazwa na kuwa balozi wa PSPF katika kata ya Kipunguni mara baada ya fainali iliyohusisha timu ya Sukuma Land FC na G Unity Fc na hatimaye timu yaG Unity kuibuka kinara kwa bao 5 kwa2 katika fainali iliyopigwa katika kiwanja cha Kipunguni B.

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma alikabidhi jezi za kuchezea fainali kwa timu mbili zilizo fuzu kuingia katika fainali hizo ambazo ni G Unity Fc na Sukuma Land FC alisisitiza wachezaji wote kuweza kijiunga na mfuko wa pensheni wa PSPF.

Fainali hizo za mashindano hayo ya ligi ya madereva bodaboda wa Kipunguni ambayo yaliweza kuhitimishwa na Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde ambapo aliweza kuwaasa vijana waweze kujihusisha na kufanya kazi kwa bidii na kuweza kuhifadhi mafao yao katika mfuko wa pensheni wa PSPF.

Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa naye alitoa neno kuhusu usalama barabarani na kuwashukuru wachezaji kwa kucheza ligi hiyo kwa usalama na kumalizika kwa amani na hata hivyo aliwasisitizakuwa watu wote wanaotumia vyombo vya moto kuwa makini pindi wawapo barabarani.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...