Skip to main content

UN YAFANYA USAFI SOKO LA TEMEKE STEREO KUADHIMISHA MIAKA 70




Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) kabla ya kuanza zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Na Mwandishi wetu

KATIKA kuadhimisho miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa walijumuika na wakazi wa Temeke katika kufanya usafi kwenye soko la Temeke Stereo.

Shughuli hiyo wameifanya baada ya wiki iliyopita kufanya shughuli za upandaji miti katika miteremko ya mlima Kilimanjaro. Wakiwa katika miteremko ya milima Kilimanjaro walipanda miti 2,000.

Shughuli hizo za kufanya usafi ambazo ziliongozwa na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, zilifanyika katika juhudi za kuleta uhalisia wa utunzaji wa mazingira kama umoja huo unavyofanya.

Akizungumza katika shughuli hizo Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kusherehekea miaka 70.

“Nachukua nafasi hii kupongeza watu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kufanya shughuli mbalimbali kuelekea maadhimisho ya miaka 70 kwa kupanda miti 2,070 kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro na hili tendo la leo la usafi kama mwendelezo wa kaulimbiu inayohimiza utunzaji wa mazingira ya“ Sayari moja, watu bilioni 7: Ulinzi wa mazingira ni wajibu wetu,” alisema.

Akisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na usafi, Mkuu huyo wa wilaya alisema wajibu wa kutunza mazingira ni wa kila mtu.



Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ikiwemo kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa wananchi na wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo mwishoni mwa juma. Kushoto ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini, Patric Otto. Wa tatu kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Temeke, Sophia Mjema, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira manispaa ya Temeke, Ally Hatibu.

“Kutunza mazingira si wajibu wa mtu mmoja. Ni wajibu wako kama ilivyo kwa jirani yako. Kunapokuwepo na watu wengi mara nyingi hutokea watu ambao hawajali wala kuona umuhimu wa kutunza mazingira, umuhimu wa kufanya haya.

“ Nawaomba wote mlioshiriki katika shughuli hii leo kuwa watu wa kuchunga mazingira katika maeneo yenu mnayofanyia kazi na majumbani kwenu.Hakikisheni mnafundishana na majirani zako katika suala hili na kuhakikisha kwamba kila mmoja anayekuzunguka anawajibika katika kutunza mazingira.”

Akisisitiza menejimenti ya mazingira, Rodriguez, alizungumza kwamba mabadiliko ya tabia nchi na mazingira endelevu ndio ajenda kuu katika malengo endelevu ya maendeleo (SDG’s).

“Mwaka huu jumuiya ya kimataifa itakubaliana kuhusu SDGs na kukamilishwa kwa malengo ya milenia (MDGs). Malengo ya milenia yamewezesha kupatikana kwa mabadiliko makubwa katika kukabiliana na umaskini, afya bora na kiwango kikubwa cha watu wanaojiunga na shule. Mataifa ya Umoja wa Mataifa kwa kupendezwa na mafanikio ya MDGs sasa wanataka kukubaliana kuhusu SDGs.

“ SDG itakuwa na vipengele 17 kikiwamo cha mabadiliko ya tabia nchi. Umoja wa Mataifa umechagua suala la mabadiliko ya tabia nchi kuwa ndio kipaumbele cha mwanzo kwani imebaini kwamba ni tishio kwa maendeleo endelevu. Hii inatokana na ukweli kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli na ni vyema kila mtu kuwajibika ili kuhakikisha mazingira yetu yanaendelea kuwa mazuri-tukianzia na mazingira yetu yanayotuzunguka” alisisitiza.

Rodriguez alizitaka jamii mbalimbali kutoa kiipaumbele katika kusafisha mazingira na usafi binafsi hasa kipindi hiki ambapo kumezuka ugonjwa wa Kipindupindu kwa mikoa ya Dar es salaam na Morogoro.

“Usafi wa soko hili ni muhimu kwa ajili ya afya yako na uhai mrefu. Afya njema inatuwezesha kuendelea kufanya shughuli zetu mbalimbali za kuchangia ukuaji wa uchumi.Hebu angalia pembeni mwako imetuchukua saa chache kusafisha soko la Temeke na je hamuoni tofauti? Nawaomba wakazi wa Temeke na wafanyakazi wa soko hili kufanya shughuli hizi kila siku kwani maisha yao, afya yao na uchumi unategemea soko hili.”

Pia aliwaalika wananchi wote katika sherehe za miaka 70 za Umoja wa Mataifa zitakazofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Oktoba 13 ili kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Pia alihimiza serikali kuendelea kuelimisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabia nchi.



Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Temeke, Sophia Mjema akitoa nasaha zake kwa wananchi na wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo, ambapo aliwataka kuzingatia usafi wa maeneo yao ya biashara pamoja na majumbani ili kuepeukana na mlipuko wa Kipundupindu.

Katika hafla hiyo ya kusafisha soko la Temeke, Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania kwa pamoja walitoa vifaa vya kufanyia usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 10. Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa menejimenti ya soko la Temeke.

Watu wengine walioshiriki katika shughuli hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy; mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Sophia Mjema, akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na maofisa wengine wa serikali na wakazi wa Temeke.

Balozi Mushy katika risala yake ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya usafi aliitaka jamii kutambua kwamba usafi ni jukumu la kila mmoja wetu kwani bila usafi madhara yake ni makubwa ikiwamo ya kutunzwa kwa mazingira.

Alilitaka jiji la Dare s salaam ambalo linalinganishwa na majiji mengine duniani kama Nairobi, Kenya; Pretoria Afrika Kusini, Washinton DC na Paris kujifunza kuwa wasafi kwani hata mlipuko wa sasa wa Kipindupindu ni dalili tosha ya kukosekana kwa usafi.

Aidha alisema kwamba suala la usafi si lazima kwenda kujifunza nje kwani ipo miji na mikoa misafi ambayo inaweza kuulizwa wamefanikishaje jambo hilo. Aliitaja miji hiyo ni Moshi, Iringa na Mwanza.

Alisema katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, wameamua kufanya usafi wa mazingira katika soko la Temeke kuonesha kwamba inawezekana kufanya usafi kwa kuwajibika kwa lengo la kufanya mazingira yawe masafi na ya uhakika.

Kwa kutekeleza usafi kwa maana nyingine kutasaidia kuondoa gharama zinazoambatana na uchafu wa mazingira.

Alitaka kila mmoja katika soko hilo kuanzia wakulima hadi wachuuzi kuwajibika kwa usafi ili mazingira yawe salama.



Pichani juu na chini ni wafanyabiashara wa Soko la Temeke Stereo, wananchi na wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa Wziara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke (hayupo pichani).









Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akikambidhi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto) vifaa vya kufanyia usafi katika Soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.



Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akivaa 'gloves' tayari kushiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.



Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakifanya usafi katika maeneo ya wafanyabiashara katika soko la Temeke Stereo.



Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akibeba taka katika soko la Temeke Stereo.



Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema wakishiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya kusheherekea maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.



Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakijumuika na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakiendelea na zoezi la usafi.







Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina (kulia), Beatrice Mkiramweni pamoja na Jacqueline Namfua wakifanya usafi kwenye maeneo ya soko la Temeke Stereo.



Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina akishiriki zoezi la kuzoa taka katika soko la Temeke Stereo.





Umoja ni Nguvu: Wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje wakishirikiana kwa pamoja kufanya usafi katika soko hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.



Petra Karamagi na Nasser Ngenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wakishikishiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo.



Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano alipomulikwa na kamera ya Modewjiblog





Zoezi likiendelea.



Zoe Glorious katika ubora wake.



#HapaKaziTu ......Usia Nkhoma Ledama akiwajibika katika zoezi la usafi soko la Temeke Stereo.



Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wafanyabiashara wakishirikiana katika zoezi hilo.







Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) akiteta jambo na na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walioshiriki kwenye zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika soko la Temeke Stereo.





Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...