Skip to main content

CCM MAFINGA MJINI CHA ZOA WANACHAMA 50 KUTOKA CHADEMA


Mgombea Ubunge Jimbo la Mafinga mjini akinadi sera na ilani za chama chake jana mjini Mafinga katika uzinduzi wa kampeni za ubunge.


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mafinga Mjini ambalo ni jimbo jipya la uchaguzi kimezoa wanachama wapya kutoka Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge zilizofanyika katika viwanja vya Mashujuu jana.


Wanachama hao wapya walikabidhiwa kadi za chama hicho na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatangu ambaye alikuwa mgeni rasmi.


Wanachama huo wapya wakiongea na Nipashe muda mfupi baada ya kukabidhiwa kadi za CCM kwa nyakati tofauti walisema wameamua kutoka CHADEMA na kujinunga na CCM kutokana sababu nyingi kubwa ni chama cha CHADEMA kuendesha siasa za kuhamasisha vujo.

Walisema kuwa wamechoshwa na maneno na vitendo vya Mgombea urais kupitia Chadema Edward Lowassa na makada wenzake wa CHADEMA na vyama shirika vya UKAWA toka wameanza kampeni katika maeneo mbalimbali ya nchi na kwa nyakati tofauti zimejaa ghiriba na ubaguzi uliokithiri. 

Waliendelea kusema kuwa tabia hizi za Lowassa ni moja ya sababu iliyopelekea CCM kutompa nafasi ya kugombea kupitia Chama hichi.

Mgombea ubunge jimbo la Mafinga mjni Cosato Chumi Jumapili wiki iliyopita alizindua rasmi kampeni zake za kuwania ubunge katika jimbo hilo mpya la Mafinga mjini ambalo limemegwa kutoka Jimbo la Mufindi Kaskazini na Tume ya Uchaguzi ya taifa (NEC). 

Chumi alisema atahakikisha anasimamia vyema ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo imekidhi mahitaji ya watanzania na amewataka wakazi wa Mafinga kutofanya makosa kwa kumpitisha mgombea kutoka vyama vingine kwani watapelekea kudumaza maendeleo ya Mafinga mjini. 

Aidha Chumi amesema endapo wananchi watamchugua pamoja na madiwani wa CCM watawapa nguvu na kupelekea maendeleo hasa utatuzi wa tatizo la maji ambalo limetokana na kuongezeka kwa idadi ya watu.




Mgombea ubunge jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akikabidhiwa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu.


Pia amesema usalama wa raia ni muhimu atahakikisha vituo vya polisi vinaongezwa katika kila kata hili kuongeza usalama pia amevitaja vipaumbele vifuatavyo endapo wakazi wa jimbo la Mafinga mjini watampa kura za ndio yeye, madiwani wote wa CCM pamoja na mgombea Uraisi wa chama hicho JOHN POMBE MAGUFULI ambavyo ni pamoja na kuongeza vituo vya afya, kuboresha elimu pamoja na mikopo kwenye vikundi vya kina mama.




Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa


Aidha mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Jesca Msambatavangu amesema Ilani ya chama ni mkataba kati ya CCM na watanzania kwa sababu imechukua mipango ya maendeleo tangu CCM imeanza kuitawala nchi hadi mwaka 2025.


Ambapo amesema mipango hiyo imebeba mahitaji yote ambayo watanzania wanahitaji kutokana na serikali kutambua idadi ya watanzania kuongezeka kila mwaka.

Hata hivyo, Msambatavangu alisema CCM ni chama ambacho kinasimamia demokrasia, usawa na amani ya Tanzania tangu nchi ipate uhuru na kuwa ahidi watanzania endapo wataichagua CCM kushika dola watasimamia muungano.


wakazi wa Mafinga mjini wakifwatilia kwa kina tukio la uzinduzi wa kampeni hizo jana.






Wananchi wa Mafinga mjini wakimpokea mwenyekiti wa chama cha CCM mkoa wa Iringa jana mjini mafinga






Waliokuwa wanachama wa CHADEMA wakikabidhiwa kadi za chama cha mapinduzi CCM na mwenyekiti wa chama hicho mkoa baada ya kujiunga na chama hicho jana mjini Mafinga.




Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...