Skip to main content

DK SLAA AMWAGA MANYANGA RASMI, AACHA SIMANZI UKAWA



DAR ES SALAAM: Na Habib Shaban
KATIBU mkuu wa CHADEMA Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema aliamua kuachana na CHADEMA na siasa kwa ujumla tangu tarehe 28/08/2015 baada ya Mbunge wa Monduli Edward Lowasa kujiunga na CHADEMA, kwa kile alicho dai kuwa asingeweza kushiriki kumsafisha mtu mwenye madhambi na badala yake aliona ni vyema ajiengue kwakuwa yeye sio muumini wa siasa za ulaghai.

Dkt Willbraod Slaa. Picha na Moshi Shaban Mallema

Kauli hiyo ameitoa katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, amabapo amesema ameamua kayasema hadharani kwa kile alicho dai kuna upotoshwaji unao endelea kuwa yuko likizo na kwamba atajiunga na shughuli za chama hicho mbele ya safari, huku akidai kuwa hakuwa likizo na wala hakupewa barua yoyote ya likizo.

Hata hivyo amesema alijaribu mara kadhaa kuandika baraua za kujiuzuru lakini hakuweza kusikilizwa na mtu yoyote, na baadae aliamua kuchukua uamuzi wa kuchana shughuli za chama hicho, na kwamba uvumi uliokuwa ukiendelea kuwa Slaa amezuiwa na mke wake Josephine.

Ameongeza kuwa kitendo cha kuwaruhusu baadhi ya wabunge waliotemwa na CCM baada ya kura ya maoni nacho kimechangia kumuondoa katika chama hicho, huku akimtolea mfano Waziri mkuu wa wazamani Fredrick Sumaye kuwa ndiye mtu ambaye alikuwa na mgogoro nae baada ya kumuita fisadi katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amabapo na yeye leo hii ameendelea kuwaita ni “MAKAPI” .

Naondoka leo huku nikisikitika kuwa sura ya CHADEMA imebadilika nakuwa kama CCM, sasa utawezaje kuleta mabadiliko nawatu wale wale wanaotuhumiwa na kashfa zinao umiza taifa hili? Alisema Dkt Slaa.

Aidha alimaliza kwa kusema amestaafu siasa ila hana chama chochote ila bado ataendelea kuwatumikia watanzania kwa njia nyingine kwakuwa ana vipawa alivyo barikiwa na mungu lakini amewataka wananchi kuto pumbazwa na shamra shamra zinazo endelea badala yake wananchi wanatakiwa kutambua kazi waliyo nayo kwa sasa.

KUHUSU LOWASA KUHUSIKA NA RICHMOND DKT SLAA AME ANIKA HAYA.

kifungu cha 152 cha katiba ya nchi hii kina sema jukumu kubwa la waziri ndio msimamizi wa shughuri za serikali sasa anawezaje kukataa kuwa yeye hakuhusika?

Na katika makampuni yaliyo omba zabuni ya Umeme mwaka 2006, kampuni ya Ricmhond ndiyo kampuni pekee iliyokuwa na sifa “sifuri” haya yoote anayajua na kama hajui basi alikuwa ni mzembe! na kama alikuwa mzembe basi hafai kuwa Rais. alisema Dkt Slaa.

Na aliagiza tenda ifanyike ndani ya siku 10, wakati sheria ya PPRA ina tamka tenda yoyote inatakiwa ifanyike ndani ya siku 45, ni kinyume na sheria.

Sasa hao wanao mtetea watoke hadharani kama mnaona sisi hatujui chochote, mbona mnatakutupumbaza!?

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...