Skip to main content

PAWAGA YATAPIKA JIMBO LA ISIMANI

baadhi ya umati uliofurika mkutanoni leeo

Mgombea urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk Johni Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Isimani William Lukuvi kwa wananchi katika mkutano wa hadhara Jimbo la Isimani.

Mgombea urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk Johni Magufuli akiwanadi wagombea udiwani kwa wananchi katika mkutano wa hadhara Jimbo la Isimani.


Mgombea urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk Johni Magufuli ameendelea na mikutano ya kampeni leo katika mkoa wa Iringa kwa jimbo la Isimani akielekea Mkoa wa Dodoma, Baada ya mkutano wake wa jana uliofanyika Jimbo la Iringa mjini katika uwanja wa kumbukumbu wa Samora.

Akitumia usafiri wa gari amepitia Jimbo la Isimani kwa barabara ya Iringa Pawaga alipata fursa ya kusalimiana na wananchi wa Jimbo la kalenga kata ya kiwere katika kijiji cha Kiwere, akieleke kijiji cha Kimande kata ya Itunundu, Tarafa ya Pawaga palipo fanyika mkutano wa kampeni uliohudhuliwa na wananchi wa vijiji vya kata nne za Itunundu, Mboliboli, Ilolompya na Mlenge.

katika mkutano huo mgombea huyo wa urais alisema anajua changamoto nyingi zilizopo jimbo la Isimani pamoja na juhudi za serikali ya awamu ya nne ilivyojitahidi kuzishughulikia kwa kusaidiana na Mbunge wa Jimbo hilo William Lukuvi, alisema yeye na chama chake anaahidi kutekeleza yafuatayo.

Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami kutoka Izazi, Pawaga, Mlowa mpaka Hifadhi ya Mbuga za wanyama Ruaha, Kuwapatia wafugaji maeneo ya malisho sambamba na kutatua migogoro ya Wakulima na wafugaji, Uimalishajimiundo mbinu ya Mifereji ya umwagiliaji iwe ya uhakika na kuanza ujenzi wa mifereji ambayo haijafanyiwa kazi, pia Uboreshaji wa Kituo cha Afya tarafa ya Pawagailikiwe katika kiwangocha Hospitali.

Akiongea na wananchi hao Dk John Magufuli alisema iwapo mtanichagua mimi na wenzangu kwa pamoja tutajitahidi kuendeleza amani iliopo katika nchiyetu, mtarajie serikali ya awamu ya tano ni ya wachapa kazi ikiongozwa namimi John Magufuli.

Huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutanohuo alichukua nafasi yakumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani kupitia ccm Williamu Lukuvi alisema anamfahamu vyema Lukuvi amekuwanae katika awamu nyingi Serikalini nimchapakazi, iwapomtamchagua nitashirikiana nae kutatu changamoto zote zilizopo.

Pia akiwaombea kura madiwani wa kata zote za tarafa ya Pawaga huku akiahidi serikali yake ikipata nafasi ya kuongoza nchi atahakikisha huduma za jamii kama elimu kuwa bure darasa la kwanza hadi kidato cha nne,vilevile kubolesha huduma za Afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa.

Akihitimisha mkutano huo ulioanza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 5 kasoro Mgombea ubunge wan jimbo la Isimani kupitia ccm Williamu Lukuvi alisema naomba wanapawaga msiniangushe, ifikapo October 25 mumpe kura Mgombea Urais wa CCM, Mgombea Ubunge wa CCM na wagombea Udiwani wote wa CCM.

Msafara wa Mgombea Urais ikiendelea na safari ya kuelekea Dodoma kwa njia ya Barabara yapata umbali wa km.80 ulipita vijiji vya Mboliboli, Makuka na Izazi Barabarani,ambapo Mgombea Urais alipata fursa ya kupungiana mikono na wananchi akielekea Kijiji cha Migoli kufanya mkutano wake wa Mwisho katika jimbo la Isimani linalojumuisha Tarafa za Isimani, Pawaga na Idodi.

Hatimae msafara uliwasili kijiji cha Migoli saa 5 na robo na kuanza mkutano uliohudhuriwa na wananchi wa kata za Malengamakali, Kihorogota, Nyang`olo, Izazi na Migoli wengiwao wakiwa katika sale za chama kwakuvaa kofia na fulana na Mashati yenyerangi za chama wananchihao walifanya mapokezi kwa mgombea uraisi alipofika kijiji cha Migoli katika uwanja wa Mpira uliopo kandokando ya Barabara ya Iringa Dodoma.

Kama ilivyo kawaida ya Dk Magufuli alianza kwa salamu za makabila yote na kuakiendelea na kuwakumbusha wananchi maendeleo yaliofanywa na serikali yake toka awali, huku akiwaomba kura wananchi kwa kuwakumbusha kuwa ifikapo Oktoba 25 2015 akichaguliwa yeye na wagombea wenzake toka ccm atahakikisha anatatua kero zote zinazo wasumbua wana Migoli.

Akichanganua alisema mnakero za ushuru usiona tija,usumbufu kwa waendesha Bodaboda kwamudamrefu na vitu vidogovidogo kama Samaki tengamoja,Nyanya dedembili na vinginevyovingi mimi ni tahakikisha usumbufu huo kwawajasiliamali wadogo wadogo unatoweka,hukuakieleza ataboresha Barabara ya Iringa Dodoma kwa eneo la Daraja kuu la Mtera kulifanyaliwe Bora zaidi,

Hukuakiahidi kushughulikia miradi ya Maji ambayo nikero kubwa kwa wakazi wa Isimani,Migoli na Shughuli za uvuvi kwajumla ninafahamu kwakuwaninauzoefu serikalini tena najua pesa itatokawapi na nitahakikisha kilakijiji au kitongoji kinapata milioni hamsini kwa wajasiliamali,ilikuendeleza shughuli zenukwaufanisi alisema.

Akimalizia kuhutubia Mgombea ubunge alisema anaomba kura kwake na kwa wagombea wote wa ccm huku akinasibisha jina lake na kinywaji cha Pombe ili wapigakura wasimsahau, alisema hivyo sambamba na kuwakaribisha wasanii wa Bongo muvi toka Dar es salaam waliofika mkutanoni hapo wakijitambulisha kwa majina huku wakijiita ni watumia Bajaji, katika kampeni waowanafika kila mahala kutafuta kura. 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...