Skip to main content

TASAF WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UWAZI NA UWAJIBIKAJI


Picha na Maktaba


Wasimamiaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini mkoani Iringa wametakiwa kuimarisha uwazi, uwajibikaji na kuruhusu makundi tofauti kushiriki kwa kutumia mfumo madhubuti wa wanufaika.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya kujenga uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya III iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Valentine mjini Iringa na kusomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Seleman Mzee.

Masenza alisema “ni mategemeo yangu kuwa utekelezaji wa mpango huu wa kunusuru kaya masikini utaimarisha uwazi, uwajibikaji na kutoa fursa kwa makundi mbalimbali kushiriki kwa kutumia mfumo madhubuti wa kubaini walengwa katika vijiji na mitaa yetu”. 

Alisema muundo wa awamu ya tatu, umezingatia vema changamoto ambazo zilijitokeza katika utekelezaji wa awamu ya pili. 

Alisema kwa maana hiyo usimamizi na ufuatiliaji umeimarishwa katika ngazi ya mkoa, halmashauri na kata kwa kuhusisha watumishi zaidi kufuatilia shughuli za mfumo wa maendeleo ya jamii. 

“Napenda kusisitiza azma ya serikali ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo na ndiyo lengo la kuanzisha mpango huu ambao utatekelezwa katika vijiji na mitaa yetu ili kuondoa umasikini kwa manufaa ya jamii yetu” alisisitiza Masenza.

Akiongelea utekelezaji wa mpango huo, mkuu wa mkoa alisema kuwa utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kuwafikia wastani wa walengwa 6,500,000 katika kaya masikini na zilizo katika mazingira hatarishi 1,000,000 za Tanzania. 

Alisema viongozi wanao wajibu wa kusimamia vizuri mpango huo ili kuhakikisha kaya zilizotambuliwa na kuandikishwa kwenye orodha ya kaya masikini, zinafaidika kwa kushiriki katika program ya uhawilishaji fedha, program ya mradi ya ujenzi ambayo itatoa fursa za ajira za muda katika kipindi cha hari, program ya kujenga uwezo wa kujikinu na kuongeza kipato na kujengewa uwezo.

Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa TASAF, Richard Njalika alisema kuwa mpango wa kunusuru kaya masikini umepangwa kutekelezwa kwa awamu ili kufikia jumla ya halmashauri 169 za Tanzania. 

Awamu za utekelezaji mpango huu zimelengwa kujenga uwezo kwa wawezeshaji wa kutosha na kujenga mifumo pamoja na kuboresha utekelezaji katika kila awamu. Alisema kuwa awamu hii imepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 katika awamu mbili za miaka mitano mitano. 

Alisema kuwa utekelezaji wa mpango unahitaji uwekezaji mkubwa kwenye mifumo na kujenga uwezo katika ngazi zote za utekelezaji.

Akiongelea sehemu za mpango huo, mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa TASAF alizitaja sehemu hizo kuwa ni kujenga uwezo katika ngazi zote za utekelezaji na kujenga na kuboresha miundombinu inayolenga sekta za elimu, afya na maji. 

Seheumu nyingine ni uhawilishaji fedha, ambapo unatoa ruzuku kwa kaya masikini sana zinazotambuliwa kwa mchakato unaoshirikisha jamii. 

Kuongeza kipato kwa kaya masikini kupitia uwekaji akiba na shughuli za kiuchumi ili kuboresha maisha. Eneo lingine ni kutoa ajira kwa kaya masikini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa hari.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...