Skip to main content

TPHA CHATOA ELIMU DHIDI YA KUPAMBANA NA TUMBAKU KWA VIJANA WADOGO DAR


Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga akizungumza wakati akifungua kongamano hilo lililo washirikisha wadau mbalimbali kwa kutoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku. (Picha na Geofrey Adroph).




Na Andrew Chale

[Dar es Salaam] Chama cha Afya ya Jamii nchini (TPHA), kimeendesha kongamano maalum kwa wanafunzi wa shule msingi zaidi ya Saba ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kutoa elimu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa bidhaa za Tumbaku pamoja na kujikinga na athari zake mbaya baadae.

Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi.

Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani, aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe.

Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia.

“Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa katika maisha yao ya baadaye.

Tukiweza kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi watakapojitambjua nafsi zao na kuamua mambo ya busara na salama katika maisha yao ya baadae” alibainisha Dk. Maegga.





Mshauri wa masuala ya Afya na Familia, mgeni rasmi Dk. Ali Mzige akizungumza kwa kutoa elimu kwa miongoni mwa watu walio weza kuhudhuria kongamano hilo la uelimishaji kuhusu Tumbaku na matumizi ya yanayotokana na bidhaa za Tumbaku.Kwa upande wake, Dk. Ali Mzige mganga wa hospitali ya kimataifa ya Afya ya uzazi ametoa elimu kwa vijana hao na kubainisha kuwa sigara, tumbaku, shisha, ugoro na kuberi ni hatari kwa afya za mwili huku ikisababisha magonjwa mbalimbali.Miongoni mwa magonjwa hayo yatokanayo na matumizi ya sigara ambapo wanaoathirika zaidi ni vijana kwa sababu ya kufuata mkumbo pamoja na kuhisi kwamba uvutaji wa sigara unaongeza sifa ya kuwa mwanaume kamili kitu ambacho si kweli.Changamoto kubwa ni kwamba serikali imeshindwa kudhibiti watengenezaji wa Sigara kwa sababu wanapata kodi kutoka katika viwanda vya sigara japokuwa mapato ni madogo kuliko madhara.




“Sigara ina kemikali 4000 ambazo zina uwezo wa kusababisha magonjwa zaidi ya 40, ambayo ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kisukari, na saratani ya mapafu, saratani ya kinywa na mengine mengi.




Tumbaku na Sigara zote zimekuwa na madhara yanayofanana. Tumbaku imekuwa ikitumika hasa maeneo ya vijijini na sigara watumiaji wengi wanatoka mjini” alieleza Dk. Ali Mzige.




Kwa upande wao wanaharakati wa kupambana na matumizi ya sigara kutoka chuo cha Tiba Muhimbili, kupitia taasisi yao ya African Fight Cancer, Bernard Temba amewaelezea wannafunzi hao kuwa, ni wakati wa kuepuka vishawishi dhidi ya watu wanaotumia sigara kwani wasipofanya hivyo wataweza kupata madhara makubwa ya kiafya.









Mwalimu Margareth William mshereheshaji katika siku hiyo ya kongamano la uelimishaji vijana kuhusu Tumbaku na madhara yatokanayo na bidhaa zake.




Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Makumbusho ambaye pia alikuwa mgeni katika kongamano hilo, alitoa wito kwa walimu na wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao ikiwemo kufuatilia nyendo zao mara kwa mara ili kuwakinga na vishawishi hivyo vya matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku kwani zina madhara makubwa hasa kwa afya za watoto wadogo.




Mradi huo wa ’80 Children Strong’, unaosimamiwa na Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) unafadhiliwa na Shirika dogo la Conquer Cancer Foundation ambalo linahusiana na American Society for Clinical Oncology (ASCO) ya nchini Marekani (Chama cha kitabibu cha masuala ya uchunguzi wa tiba ya saratani.




Hata hivyo, TPHA imedhamiria kuwa kila mtoto anapata haki ya kuelimishwa kujikinga na matumizi hayo mabaya ya tumbaku, ambapo kwa darasa la watoto 80, asiwepo hata mmoja atakayeingia kwenye viashiria vibaya vya matumizi ya tumbaku hivyo wataendelea kutoa elimu hiyo sehemu mbalimbali nchini.




Kwa upande wa shule hizo zilizohudhuria kongamano hilo ni pamoja Shule ya Msingi Mapambano, Kijitonyama Visiwani, Victoria, Mwananyamala B, Mwananyamala Kisiwani, Mashujaa, Shekilango na Mapambano.




Kwa upande wa watoto hao walipata pia wasaha wa kuuliza maswali na kupatiwa majibu huku pia kukifanyika na masuala ya maigizo, ngoma, shahiri na ngonjera zilizokuwa na jumbe mbalimbali za kupambana na matumizi ya tumbaku.









Wanafunzi wakisoma na kuelekezana jarida lililochapishwa mahususi kwa ajili ya kuelimisha matumizi mabaya ya Tumbaku.














Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mashirika na vyuo mbalimbali.









Kikundi cha majigambo ya jukwaani (ngonjera) kikitoa ujumbe kwa wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wenzao kuhusiana na kupambana na kudhibiti matumizi hatari ya Tumbaku.











Wanafunzi wakionesha vipaji vyao vya kuigiza kwa kuelimisha kuhusiana na na madhara ya Tumbaku na ni namna gani ya kuweza kujikinga.









Bernard Temba kutoka Chuo cha Afya cha Muhimbili akitoa somo kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizohudhuria kongamano hilo lililofanyiaka katika shule ya Msingi ya Kijitonyama Kisiwani









Shairi mahususi likiimbwa na wanafunzi hao likiwa limebeba ujumbe wa kijana jiepushe na matumizi ya Tumbaku na bidhaa zitokanazo na Tumbaku.









Mwanafunzi wa darasa la tano, Tadei Ladislausi kutoka shule ya msingi Shekilango (kulia)akisoma madhara yanayo wakumba watumiaji wa Tumbaku.








Wawili kulia ni wanafunzi kutoka Chuo cha Afya Muhimbili, kushoto ni wanafunzi wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani wakiwa wanasikiliza kwa makini maada zilizo kuwa zikiendelea katika kongamano hilo.











Wanafunzi wakiuliza maswali kwa watoa mada inayo husiana na afya kwa kijana na kuepuka matumizi mabaya ya Tumbaku









Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani, Bw. Charles Nombo akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi.









Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioweza kuhudhuria katika kongamano hilo.









Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii Bi. Elizabeth Nchimbi akitoa nasaa kwa vijana walioweza kuhudhuria na wale walioko nje wasiweze kutumia Tumbaku kwani ni hatari kwa afya za binadamu









Waandhishi wa habari wakiwa kazini.









Afisa Elimu kata ya Kijitonyama, Mwalimu Shangwe Temba akifunga kwa kutoa neno kwa vijana kuacha kujiingiza katika makundi mbalimbali kwani ndio yanayo pelekea vijana wengi kuhamasika na kuanza kutumia Tumbaku ambayo huwaletea vijana wengi matatizo hususani kwa wanafunzi kuacha shule kwa kuugua vifua vikuu na magonjwa mengine mengi









Picha ya umoja wa kikundi cha wanafunzi kinacho elimisha matumizi mabaya ya bidhaa zinazotokana na Tumbaku.








Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...