Skip to main content

CHAVITA IRINGA WAOMBA KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UCHAGUZI



Katibu wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Iringa, Shaibu Juma Shaibu akiongea na SIMBAYABLOG  jana. (Picha na Friday Simbaya)


Wakati zikiwa zimebakia siku chache kabla ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu watu wenye ulemavu mkoani Iringa walalamikia vyama vya siasa pamoja na tume ya taifa ya uchaguzi nchini (NEC) kwa kutowekewa mazingira mazuri kushiriki mchakato wa uchagauzi mwaka huu.

Akizungumza na SIMBAYABLOG katika mahojiano maalumu na Katibu wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Iringa, Shaibu Juma Shaibu ili kutakakujua namna gani vyama vya siasa na tume ya uchaguzi (NEC) vinawashirikisha.

CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) ni mmoja wa mwanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA).

Katibu huyo alisema watu wenye ulemavu mkoani hapa hawashirikishiwi kikamilifu katika masuala uchaguzi tangu kampeni hizo zianze.

Alisema kuwa wao kama walemavu hawajui sera za vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mwaka huu.

Alisema kuwa wao kama walemavu wasiona hawajapata fursa yakushiriki katika kampeni za uchaguzi kutokana na vyama vya siasa kutowapa kipaumbele katika masuala ya mchakato wa uchaguzi.

Alisema kuwa vyama vya siasa vinapaswa kuweka wakalimani katika mikutano yao ya kampeni ili wapate tafsiri ya kinachozungumzwa kwa lugha ya alama (sign language).

Aliongeza kuwa mbali na watu wenye ulemavu wa kuona, wapo pia walemavu mbalimbali mkoani lakini vyama hivyo havijaweza kuwashirikisha kikamilifu.

Alitoa mfano kwamba Chama cha Viziwi wanachama wake wengi walihamasika katika mchakato wa kujiandisha katika daftari la wapigakura mwaka huu, lakini wengi wao hawajashiriki katika kampeni zinazoendelea kutokana na kukosa ushilikishaji ikiwemo kutokuwepo kwa wakalimani kwenye mikutano yao.

Alisema wanachama wengine wamekuwa wakimzonga kuhusu kusaidiwa kupatiwa wakalimani, lakini kutokana na ukata wa chama hicho wanashindwa kuweka mkalimani kila sehemu.

Alisema kwa mfano, kuweka mkalimani katika kampeni unatakiwa kumlipa wastani ya shilingi laki moja kwa masaa 12.

Alisema kiwango hicho cha pesa cha kumlipa mkalimani ni kikubwa sana kwa chama chao kuweza kulipa gharama hizo.

Kwa mujibu wa katibu huyo mkoa wa Iringa unazaidi ya watu wenye ulemavu (PWDs) 500.

Alisema kati ya walemavu hao ni wanafunzi katika ngazi mablimabli na wengine ni wafanyakazi katika sehemu mbalimbali na wengi wao wamejiandikisha kupigakura mwaka huu.

Kwa upande wa serikali kupitia tume ya uchaguzi, katibu huyo alisema serikali pia haijawaka mazingira mazuri kwa ajili ya walemavu.

Kwa mfano, alisema kuwa mpaka sasa wao kama viziwi na walemavu wengine hawajapatiwa elimu ya uraia ya namna watakavyoshiriki kupigakura.

Alisema kuwa vituo vya kupigia kura ni lazima viweke mazingira mazuri yakuwawezesha kupigakura kama watu wenye ulemavu.

“Watu wenye ulemavu tupo wengi kwa mfano, walemvu wa viungo, wasiona na wenye ualbinism, vituo vya kupigiakura havijaweza kuweka wakalimani kwa ajili ya viziwi, hawaweka mazingira kwa walemavu wa viungo na wasiona pia hakuna karatasi maalumu ya nuktanundu kwa ajili ya kupigakura,” alisema Shaibu.

Nipashe pia ilifanya mahojiano na baadhi ya wagombea ubunge wa Jimbo la Iringa mjini kuhusiana na tuhuma hizo za walemavu kutoshirikishwa kwenye kampeni.

Mmoja wa wagombea hao kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Mch. Peter Msigwa alisema kuwa suala la kushirikishwa katika kampeni ni la serikali sio ya vyama vya siasa.

Alisema kuwa wao kama chama cha siasa wanachofanya ni kuikubusha serikali iweka mazingira mazuri kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Alitoa mfano kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Iringa mjini na kukamata halmashauri hiyo, watahakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa ajili ya walemavu pamoja na kuwajengea mabanda maalumu kwa ajili watu wenye ulemavu.

Pia alisema kuwa watunga sheria ndogondogo kwa ajil;I ya kuwalinda watu wenye ulemavu hususan wakati wakupanda mabasi.

Kwa upande wake, mgombea ubunge kupitia ACT Wazalendo Chiku Abao alikiri kutowashirikisha watu wenye ulemavu kwenye kampeni za uchaguzi, lakini wanachofanya ni kuwasemea kwenye majukwa.

Alisema kuwa watu wenye ulemavu mambo yao yamewekwa kwenye ilani katika kuweka mikakti kama makundi maalumu wenye mahitaji maalumu.

Hata hivyo Jimbo la Iringa mjini ni vyama vitano vilivyosimamisha wagombea kuwania kiti cha ubunge ambavyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM), ACT Wazalendo, DP, ADC na Chadema.

Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Amina Molel, jumuiya hiyo iliomba sheria ya haki za watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 ifanyiwe marekebisho ili kuweza kulipa baraza la taifa la watu wenye ulemavu meno.



“Baraza linataka kuratibu, kusimamia na kutekeleza masuala yetu likiwa chombo huru badala ya kuwa chombo cha ushauri tu chini ya utendaji wa kamishna wa Idara ya Ustawi wa Jamii ambaye kwa nafasi yake ana majukumu mengi,” Molel alisema.









Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...