Skip to main content

BREAKING NEWS....Mwenyekiti wa NLD, Emmanuel Makaidi afariki dunia



Dk. Emmanuel Makaidi enzi za uhai wake.

MWENYEKITI Mwenza wa Ukawa na Mwenyekiti wa chama cha NLD, Emmanuel Makaidi amefariki dunia leo mchana kwa shinikizo la damu akiwa Hospitali ya Nyangao mkoani Lindi.

Wasifu wake

Alizaliwa Aprili 10, 1941 huko wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Alianza elimu katika Shule ya Msingi Namalenga wilayani Masasi kati ya mwaka 1948 – 1952, mwaka 1953 – 1954 alisoma katika Shule ya Kati (Middle school) iitwayo Luatala hukohuko Masasi. Baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari ya Chuo cha Mtakatifu Joseph na kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne kati ya mwaka 1953 hadi 1956.

Makaidi alisoma darasa la 13 na 14 (kidato cha tano na sita) katika Shule ya Sekondari Luhule, Uganda kati ya mwaka 1957 – 1958.

Baada ya hapo alielekea Afrika Kusini na kujiunga na Chuo Kikuu cha Witwatersrand na kuhitimu Shahada ya Uendeshaji na Usimamizi kati ya mwaka 1958 – 1960.

Baada ya kuhitimu vizuri pale Witts, aliendelea kupata ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili, mara hii alielekea Marekani na kusoma masuala ya Menejimenti na Utawala kwa ngazi ya uzamili kati ya mwaka 1960 – 1962. Alisoma pia katika Chuo Kikuu cha Howard kilichoko jijini Washington, Marekani.

Baada ya kurejea nchini akiwa mhitimu wa M.A, Makaidi alianza kazi serikalini mwaka 1966 hadi mwaka 1973 akiwa mchambuzi kazi mkuu, katika kitengo cha Utumishi.

Kati ya mwaka 1974 na 1975 (miaka miwili). Alirudi tena Marekani na kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Howard.

Aliporejea nchini kwa mara ya pili mwaka 1976 aliendelea na kazi yake pale Utumishi hadi mwaka 1985 alipopewa kazi nyingine kubwa zaidi, akawa Mkurugenzi wa Miundo na Mishahara kwenye kamati iliyokuwa inashughulikia mashirika ya umma nchini.

Baada ya hapo aliendelea na kazi serikalini ila kuanzia mwaka 1992 hadi mauti yanamfika, Dk Makaidi hajajishughulisha tena na kazi za serikalini wala mashirika binafsi. Alikuwa amejiajiri akiwa na kampuni kadhaa zilizoajiri Watanzania wa vipato vya kawaida, lakini pia alikuwa akitoa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa kampuni za ndani na nje ya nchi huku akiongoza chama cha NLD akiwa Mwenyekiti.

Dk Makaidi ni mwandishi mzuri wa vitabu, ameshaandika zaidi ya vitabu 10.

Marehemu ameacha mke aitwaye Modesta Ponela na walibahatika kupata watoto wanane.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi . AMEN!

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...