Skip to main content

JUMLA YA WATU 526,006 MKOANI IRINGA KUPIGAKURA UCHAGUZI MKUU


Kaimu wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Selemani Mzee (katikati) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo akifungua mdahalo wa wazi juu ya amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu unaofanyika katika ukumbi wa chuo Kikuu Huria (OUT)mjini Iringa. Kutoka kushoto walioketi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilolo Martin Mlwafu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi, Mwenyekiti wa ICISO Alexander Kisinini na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa, Wilfred Myuyu. Mdahalo huo uliandaliwa na Iringa civil society organization (ICISO-Umbrella) kwa kushirikiana na Asasi ya Foundation for Civil Society (FCS) jana. (Picha na Friday Simbaya)

Na Friday Simbaya, Iringa

WAKATI zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Oktoba mwaka huu, Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa, Wilfred Myuyu amesema ameanza kupokea vifaa vya uchaguzi.

Mratibu huyo alisema hayo wakati wa mdahalo wa wazi juu ya amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) mjini Iringa jana. 

Mdahalo huo uliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Iringa Civil Society Organization (ICISO-Umbrella) kwa kushirikiana na asasi ya ‘The Foundation for Civil Society (FCS).’ 

Myuyu ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi (Sehemu ya Serikali za Mitaa) alisema kuwa baadhi ya vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na maboksi 5,995 ya kupigiakura, taa mbalimbali na daftari la kudumu la wapigakura.

Alisema kuwa uchaguzi ni mchakato na tayari Mkoa wa Iringa umeanza maandalizi na utakuwa na jumla ya vituo vya kupigiakura 1,641 na kuongeza kuwa kila kituo kitakuwa na wapigakura wasiozidi 500.

Wilfred Myuyu alisema kuwa mkoa umeandikisha jumla ya wapigakura 526,006 kwa kuvuka lengo la matarajio la 521,491 na kufikia asilimia 100.8.

“Vituo vile vilivyotumika kujiandikisha wapigakura ndivyo vitakavyokuwa vituo vya kupigiakura na kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na wapigakura wasiopungua 500 na kama kituo kile kilikuwa na wapigakura 1,000, basi kituo hicho kitagawanywa na kuwa vituo viwili vya kupigiakura ambapo vitakuwa ‘A’ na ‘B’, ” alisema Myuyu.

Alisema kuwa vituo vyote vya kupigiakura vitafunguliwa kuanzia saa 1 asubuhi na kufungwa saa 10 jioni ambapo vitageuzwa kuwa vituo vya kuhesabia kura.

Aidha, alisema kuwa orodha ya majina ya wapigakura itabandikwa siku nane kabla ya uchaguzi mkuu, ili kuwapa fursa watu kuangalia majina yao katika vituo walivyojiandikishia.

Alisema kuwa kanuni za uchaguzi mkuu za mwaka 2015 zinavitaka vyama vya siasa kuwaelimisha wanachama wake namna ya kupigakura na baada ya kupigakura hawaruhusiwi kusubiri matokeo ili kuepusha msongamano.

Mkoa wa Iringa ulianza uandikishaji ya wapigakura katika daftari la kudumu la wapigakura Aprili 29 na kukamilika Mei, 29 mwaka huu.

“Kwa mujibu wa sheria, matokeo ya udiwani yanatangazwa na msimamizi msadizi wa kata, ya ubunge msimamizi wa wilaya na urais ni tume,” alisema.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Damian Lubuva aliagiza waratibu na wasimamizi wa uchaguzi pamoja na makamanda wa polisi kutenda haki wakati wa Uchaguzi Mkuu kwa kuwa usalama wa Taifa upo mikononi mwao na kuonya kuwa kosa lolote linaweza kuiingiza nchi matatizoni.

NEC ilisema hayo katika kikao kilichohudhuriwa na wasimamizi wa uchaguzi wa halmashauri zote nchini pamoja na makamanda wa mikoa wa Jeshi la Polisi, ambalo liliongozwa na mkuu wake, IGP Ernest Mangu, pamoja na makamishna wake- Diwani Athumani (Upelelezi wa Makosa ya Jinai), Paul Chagonja (Operesheni), Mussa Ali Mussa (Polisi Jamii) na Suleiman Kova (Kanda Maalumu Dar es Salaam) pamoja na baadhi ya wakuu wa vikosi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...