Skip to main content

MAGUFULI AITEKA SINGIDA, KESHO KUNGURUMA LIVE UWANJA WA NAMFUA


Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma (hawapo pichani),alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni. PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru kiongozi huyo wa dini kwa kujitolea kumuombea Dua ya heri na afya njema katika nafasi yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida jioni ya leo ,wakati akiwaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani. 



Dkt. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali hasa za mashirika ya dini ambazo zinaendesha hospitali katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili kuimarisha huduma za kiafya kwa jamii.



Sehemu ya umati wa Wakazi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi kwenye mkutano wake wa mwisho kwa jioni ya leo,ambapo kesho anatarajia kuendelea na kampeni mkoani Singida na baadae kuhitimisha kampeni zake kwenye mkutano mkubwa ambao unatarajiwa kurushwa live na kituo cha Star TV.



Kiongozi wa Msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli,Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt.Magufuli kuwahutubia wananchi wa Ikungi jioni ya leo na kuwaomba kumpigia kura ya ndio ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchahuzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.

Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na pia kuwaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia debe Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi,mkoani Singida.
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili mjini Itigi mkoani Singida mapema leo mchana,tayari kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni mjini humo.



Baadhi ya Wazee wakifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya wananchi wa mji wa Itigi mkoani Singida mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Manyoni wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara wa Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba kura ili awe Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ambapo ameaomba ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kumpigia Kura za Urais,Ubunge na Udiwani..
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Ndugu Damiel Mtuka mara baada ya kukabidhiwa Kitabu cha Ilani ya chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana mjini Manyoni mkoani Singida
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Manyoni wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Itigi Ndugu Yahaya Omar Masele mbele ya Wakazi wa mji huo (hawapo pichani),waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Itigi Ndugu Yahaya Omar Masele mbele ya Wakazi wa mji huo (hawapo pichani),waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana.
Baadhi ya wananchi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...