Skip to main content

Mwalimu ampiga mwandishi

Mwalimu Willibroad Samson wa Shule ya Sekondari Kitunda iliyopo Wilaya ya Ilala, akimdhibiti mwanafunzi, Elia Simion aliyekuwa akipigana na mwenzake. Picha na Tumaini Msowoya 
By Mwandishi wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwandishi wa Mwananchi, Tumaini Msowoya jana alipigwa ngumi kadhaa kichwani na mwalimu wa Shule ya Sekondari Kitunda wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.
Msowoya alipigwa na mwalimu aliyefahamika kwa jina la Willibroad Samson alipokwenda shuleni hapo kufuatilia madai kwamba baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, wiki iliyopita waliandikishwa na kupewa vitambulisho vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Msowoya alisema kwamba tukio hilo lilitokea kati ya saa 4.30 na saa 5.00 asubuhi karibu na jengo la ofisi za walimu. “Nilifika shuleni pale saa 3.00 asubuhi kwa ajili ya kuonana na mkuu wa shule, sikumkuta ila nilipokewa na makamu mkuu wa shule. Lakini wakati nikiendelea na mazungumzo ofisini kwa mwalimu huyo tulisikia wanafunzi wakipiga kelele,” anasema Msowoya.
Alisema kuwa alipotaka kutoka nje baada ya kukamilisha mazungumzo na makamu mkuu wa shule alisikia kelele zikipigwa huku mawe yakirushwa na kupiga jengo la ofisi ya walimu wa shule hiyo. “Hivyo tukaufunga mlango na baada ya muda mfupi nilitoka nje na kushuhudia wanafunzi wawili wakipigana huku wenzao wakishangilia,” alisema.
Kwa mujibu wa Msowoya, alianza kupiga picha za tukio hilo, na punde alimwona mwalimu Samson akiamulia wanafunzi waliokuwa wanagombana. Pia, alimwona mwalimu huyo akimdhibiti Elia Simion, mmoja wa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliokuwa wanapigana huku akitoka damu mdomoni baada ya kupigwa na mwenzake.
Katika tafrani hiyo, Msowoya alisema mwalimu huyo alimpiga huku akimvutia katika ofisi ya walimu, lakini walimu wengine waliingilia kati kumzuia.
Kutokana na kipigo hicho, alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Kitunda ambako alipewa fomu ya PF3, kisha akapatibiwa katika Zahanati ya Kitunda.
Alipoulizwa makamu mkuu wa shule aliyejitambulisha kwa jina moja la Masatu kuhusiana na tukio hilo alikiri kushuhudia lakini akasema mwalimu aliyefanya tukio hilo anajitolea kufundisha, siyo mwajiriwa wao.
Mwalimu Samson alipoulizwa sababu za kumpiga mwandishi alisema kuwa alikasirishwa na kitendo cha kupigwa picha wakati akiamulia ugomvi wa wanafunzi. Hata hivyo, kuhusu madai kwamba wanafunzi waliandikishwa na kupewa vitambulisho kwa ajili ya kupiga kura, Masatu alikanusha akidai wanafunzi walipigwa na kupewa vitambulisho vya shule ambavyo mpigaji ni mtu binafsi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...