Skip to main content

LEAT WATOA MIZINGA 350 KWA VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI



Mkuu wa wilaya Richard Kasesela akikabidhi moja ya mizinga 175 kwa mfugaji nyuki kutoka Kiwele


Baadhi ya wafugaji nyuki wakisikiliza hotuba ya mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela. (Picha na Denis Mlowe)


NA DENIS MLOWE, MUFINDI

TIMU ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) umetoa jumla ya mizinga ya kufugia nyuki 350, kwa vikundi 16 vya wilaya ya Mufindi na Iringa vilivyoko katika mkoa wa Iringa.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa mizinga hiyo iliyofanyika katika kata ya Sadan wilayani Mufindi juzi, Afisa mradi wa LEAT kutoka Mufindi Jamal Juma alisema lengo la mradi huo ni kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kuongeza kipato cha jamii kwa njia ya kufuga nyuki na kupanda miti.
 
Alisema kuwa malengo mengine mahususi ya mradi huo ni kuleta ufanisi wa kulinda, kutunza na kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza kipato cha mwananchi mjasiriamali mara baada ya mauzo ya asali iliyovunwa kupitia mizinga hiyo.

Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache yenye utajiri mkubwa wa rasilimali za asili mathalani misitu na wanyapori hivyo kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Juma alisema kuwa kutokana na hali hiyo kuna changamoto mbalimbali za usimamizi na uhifadhi zikiambatana na uchomaji moto ovyo, kuchoma mkaa,ukataji miti uliokithiri na ujangiri mambo ambayo inasababisha hasara kwa taifa.

Alisema kuwa kutokana na changamoto hizo husababisha umaskini, kukauka kwa vyanzo vya maji kutoweka kwa uoto wa asili na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“Mradi huu utasaidia sana jamii ya watu wa wilaya ya Mufindi walioko katika vikundi vya ufugaji nyuki kuhakikisha unaboresha kipato kwa kuendesha mafunzo ya ufugaji nyuki na uvunaji, upandaji miti,kusaidia jamii kwa kuzipatia vitendea kazi vya ufugaji nyuki kama hivi ambavyo leat imetoa kwa kusaidiana na USAID utasaidia kuondokana na changamoto zote hizo endapo utafanyiwa kazi kwa umakini. “ alisema 

Alisema kuwa awamu ya kwanza ya mradi vimenufaisha vikundi 8 vyenye watu 22 vilivyoko katika vijiji vya Lugoda, Lutali, Igombalavanu, Uhimbila, Mapogoro, Utosi, Tambalang’ombe, Kibada na Nyololo katika wilaya ya Mufindi na vikundi 8 katika wilaya ya Iringa ambapo kila kikundi kimepata mizinga 22 kama mtaji

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufundi,Joika Kasunga katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Utumishi, Allan Mwela amewaasa wananchi wanaokaa pembezoni mwa misitu kuacha kufanya shughuli za uhalibifu wa msitu ikiwemo uchomaji moto kwa ajili ya uwindaji shughuli za kilimo pamoja na uchomaji wa mkaa.

Aidha amewataka wananchi wa kuitunza vizuri misitu ili kuweza kuendelea kupata mvua kwa wingi na kuondokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo kwa sasa kwani misitu inavyoathiliwa na wananchi kwa matumizi ya kila siku na kusema kuwa chanzo cha misitu hiyo kuharibika ni kutokana na wananchi wenyewe.

“Uhifadhi wa misitu sio suala la mtu mmoja au kundi moja ila la watu wote hii inatokana na ukweli kwamba madhara yatokanayo na uaribifu wa mazingira hayana mipaka na humpata kila mtu hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kushiriki katika kulinda maliasili” alisema

Aliwapongeza Leat kwa kuweza kuwasadia wajasiliamali walioko katika vikundi vya kuondokana na umaskini kwa njia ya ufugaji wa nyuki.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...