Skip to main content

Matokeo ya mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Saba 2015

 Katibu Mtendaji wa NECTA Dk. Charles Msonde

Baraza la Mitihani Tanzania - NECTA kimetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba iliyofanyika September 9 na 10 mwaka huu ambapo mikoa ya kanda ya ziwa imefanya vizuri ikilinganishwa na mikoa mingine nchini.

Akitangaza matokeo hayo jijini DSM, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk. Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 51,8034 kati ya 76,3602 wamefaulu sawa na asilimia 67.84, ambapo kati yao wasichana wamefaulu kwa asilimia 64.60 na wavulana asilimia 71.58 huku kiwango hicho cha kikiongezeka kwa asilimia 10.85 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana wa asilimia 56.99.

Dk. Monde amezitaja shule zilifanikiwa kuingia kumi bora kitaifa mwaka huu ni pamoja na shule ya Waja Springs ya Geita iliyoshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Enyamai ya Mara na Twibhoki pia ya Mara katika nafasi ya tatu huku zikifuatiwa na shule nyingine 7 zote kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. Shule ya Mwashigini ya mkoani shinyanga imetajwa kushika nafasi ya mwisho.

Katika hatua nyingine Dk. Msonde amezungumzia pia kukamilika kwa maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne ambayo itafanyika kuanzia nov mbili hadi 27 mwaka huu na kuwataka wasimamizi pamoja na watahiniwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ili kuepuka kufutiwa mitihani hiyo.

Kwa kuwa mitihani hiyo inafanyika tanzania bara na visiwani Dk Msonde amewatoa hofu watahiniwa wa Zanzibar ambako kuna hofu ya uvunjifu wa amani kutokana na masuala ya kisiasa kuwa mitihani hiyo itaendelea kama kawaida kwani suala la ulinzi limeimarishwa.


http://www.wavuti.com/2015/10/matokeo-ya-mtihani-wa-kitaifa-wa-darasa.html

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...