Skip to main content

TPHA CHAWAOMBA WADAU KUTOA USHIRIKIANO ILI KUPAMBANA NA MATUMIZI TUMBAKU KWA VIJANA



Dk. Adeline l. Kimambo(kulia) kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akitoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku mbele ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kujadili changamoto wanazokabiliwa nazo hasa wanapokuwa wanatoa huduma kwa jamii kuhusu matumizi ya Tumbaku na kuwaomba wadau hao kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo waliyojiwekea.Katikati ni Dk Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) (Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)


Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga(kushoto) akizungumza jambo kwenye kikao kilichowashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika manispaa za jijii la Dar es Salaam kuhusu kushirikiana na wadau mbalimbali hasa kutoka katika manispaa za jiji hilo ili kudhibiti matumizi na madhara ya Tumbaku hapa nchini na kusisitiza kushirikiana ili kupambana na janga hili hapa nchini linalopelekea kupoteza nguvu kazi kubwa.





Dk. Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akisisitiza wadau kujitokeza na kushirikiana nao ili kutatua tatizo la matumizi ya tumbaku pamoja na vileo hasa kwa watoto wadogo wanaoanza kutumia wakiwa wadogo na kupelekea kupata madhara udogoni.Ambapo kwa utafiti uliofanyika umeonesha asilimia 6 ya watoto 400 wa shule za msingi walianza kutumia tumbaku wakiwa hawajui madhara yake.






Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii (TPHA),Dk. Mashombo Mkamba akizungumza jambo wakati wa majadiliano ni kwa namna gani wanaweza kupunguza matumizi ya Tumbaku katika jamii unayowazunguka na hata kuwaomba wadau mbalimbali kushirikiana ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya matumizi ya Tumbaku hasa kwa watoto wadogo ambao ni nguvu kazi ya baadae.



Dk.Tulitweni Mwinuka kutoka manispaa ya Temeke akieleza changamoto wanazozipata pale wanapokuwa wanatoa elimu ya matumizi ya Tumbaku na kusisitiza changamoto kubwa wanayoipata ni wanasiasa kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa kuhofia kupoteza wapiga kura wao wakati wa uchaguzi.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...