Skip to main content

WAFANYAKAZI WA NURU FM 93.5 IRINGA WAFANYA USAFI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA IRINGA


Fredy mgunda ambaye ni chief repoter wa radio nuru fm 
hawa muhamed na devota romanus wakiwa eneo la tukio wakifanya usafi
shauri mkwawa a.k.a mama la mama na wafanyakazi wenzake wakifanya usafi



shauri mkwawa a.k.a mama la mama na wafanyakazi wenzake wakifanya usafi







Wafanyakazi wa kituo cha redio nuru fm 93.5 iringa wamejitokeza kufanya usafi katika hospital ya rufaa ya iringa kwa lengo la kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dr john pombe magufuli.


Wakizungumza wakati wakiwa wanafanya usafi katika eneo hilo wamesemakuwa wameamua kufanya usafi katika hospital hiyo kwa kuwa ndio hospital inayohudumia wananchi wengi kuliko hospitali nyingine zilizopo mkoani hapa.


Denis nyali ni mhariri wa habari wa radio hiyo amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa lengo la kuwaonyesha wananchi na wafanyakazi wa hospital hiyo kuwa iringa kuwa safi inawezekana kutokana na kauli moja tu aliyoitoa rais imekuwa gumzo kila kona hivyo wananchi wanatakiwa kufanya usafi kila mara na usafi uwe jadi yao.


“Angalia hapa leo hospitali kama hii ya rufaa uchafu wote huu unatoka hapa kama wanagekuwa wanafanya usafi kila siku na kuona usafi ni sehemu ya maisha yao tusingeona hali hii na pia tusinge pata wagonjwa wa magonjwa ya milipuko naomba wananchi wezangu zoezi hili liwe endelevu”alisema denis nyali.

Hawa muhamed na grace michaeli wamesema ni aibu wananchi kukumbushwa kufanya usafi na rais wakati huo ni wajibu wa kila mwananchi na kuongeza kuwa wanampongeza rais wa awamu ya tano kwa kasi yake anayoendana nayo sasa kwa inawafanya watanzania waanze kuiamini serikali yao tofauti na ilivyo kuwa hapo awali.


Fredy mgunda ambaye ni chief repoter wa radio nuru fm amewataka wananchi kuendeleza juhudi za rais kwa kuwa wasafi kila siku na kuafanya usafi kila mara ili nchi hii isikumbwe na magonjwa ya milipuko na kuongeza kuwa serikali ya manispaa ya iringa inatakiwa kutunga sheria ndogondogo za usafi.


“Hapa iringa hatuna kabisa sheria za usafi kwa utaona wananchi wanatupa takataka hovyo huku viongozi wa mji huu wakiwa kimya kwa namna hiyo hatuwezi kuwa na mji msafi hata siku moj,ukienda pale stand watu wanakojoa na kujisaidia hovyo lakini hawachukuliwi hatua yoyote ile “alisema fredy mgunda


Hussein faraha ni mtangazaji wa radio hiyo amewaomba wananchi kuendeleza kufanya usafi kwa kuwa ndio jadi ya mtazania hata ukikumbuka hapo zamani wakati mwalimu nyerere akiwa hai alikuwa akisisitiza usafi hivyo ujio wa rais huyu wa awamu ya tano john magufuli naanza kufananisha na marehem waziri mkuu Edward molinge sokoine kwa uchapaji kazi wake.


“Leo nimemuana rais huyu akizama kwenye matope kufanya usafi huku akiwa na sura ya furaha kujumuika na wananchi wakati wa kufanya kazi hiyo ni ishara tosha kumlinganisha na marehemu mwalimu nyerere kwani alikuwa anafanya kazi pamoja na wananchi wake”. alisema husien farahani


Naye jeni kalinga amesema kwa anamkubali sana rais kwa kasi yake na kuwaomba wananchi kumuombea awe na uhai kwa kuwa sasa anatimiza matakwa ya watanzania wengi waliokuwa wamekata tamaa na nchi yao


“Daa jamaa yangu magufuli jembe kinoma si unaona linavyolima kila kona ni gumzo hivyo lazima tumpe nguvu na serikali imuongezee ulinzi tuiseje tukalipoteza jembe letu lilorudisha matumaini ya watanznia”alisema jeni kalinga.


Kwa upande wao baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo wamekipongeza kituo hicho cha radio kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa wamejituma kufanya usafi kwenye mahodi na nje ya hodi hasa wanaume walikuwa wanadeki huku kwenye mahodi hicho ni kitendo cha kujivunia kutoka kwako.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...