Skip to main content

BACK TO LIFE SOBAR HOUSE: JAMII ISIWATENGE WAHANGA WA DAWA ZA KULEVYA




NaGeorge Binagi-GB Pazzo @BMG


Jamii nchini imetakiwa kutowanyanyapaa waathirika wa dawa kulevya badala yake wawasaidie kuondokana na matumizi ya dawa hizo ikiwemo kuwafikisha katika vituo vya utimamu wa akili (Sobar House).

Rai hiyo ilitolewa wiki hii na Eddy Darkis ambae ni Meneja wa Kituo cha Utimamu wa akili cha Back To Life Sobar House kilichopo Pasiansi Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, ambacho kinawasaidia wahanga wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Darkis alibainisha kuwa badhi ya wanajamii wamekuwa wakiwanyanyapaa waathirika wa dawa za kulevya, jambo ambalo linakwamisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Kwa mwaka 2015, zaidi wahanga 50 wa dawa za kulevya waliokuwa katika Kituo hicho kutoka Mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mkoani Mwanza, wamerejea katika hali zao za kawaida baada ya kupatiwa tiba ya kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya huku wengine zaidi ya 25 wakiendelea kupatiwa tiba katika kituo hicho.

Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu nchini
(OJADACT) Edwin Soko, Idadi ya Watumiaji wa dawa za Kulevya Jijini Mwanza imefikia zaidi ya Watumiaji Elfu Kumi katika kipindi cha miezi sita iliyopita huku sababu za ongezeko hilo zikiwa ni kutokana na kukosekana kwa njia mathubuti za kupambana na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na wanaojihusisha na biashara ya dawa hizo mara kwa mara kubuni mbinu mpya za usafirishaji jambo linalosababisha ugumu katika kupambana na biashara hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...