Skip to main content

HOYCE TEMU AFUNGA MWAKA KWA KUTEMBELEA KITUO CHA WAZEE







Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) kushoto Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye ( wa pili kulia), Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa (kulia) pamoja na mpiga picha wa kipindi cha Mimi na Tanzania, Geofrey Magawa a.k.a KIM (kushoto) wakiwasili Desemba 31, 2015 kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. 

Na Rabi Hume, Modewjiblog

Miss Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu amemaliza mwaka 2015 kwa kutembelea kituo Nunge ambacho ni makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza kilichopo Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Hoyce ambaye amekuwa akisaidia watu wa aina mbalimbali wenye matatizo ikiwa ni kama moja ya kazi wanazofanya mamiss kwa jamii pia kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho kimekuwa kikisaidia watu mbalimbali na katika halfa hiyo aliongozana na watu wake wa karibu ikiwepo kamati ya Miss Tanzania.

Katika halfa hiyo iliyodhaminiwa na Malaika Beach, Hoyce baada ya kuwasili kituoni hapo yeye na timu nzima aliyoongozana nayo walifanya shughuli za kijamii katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza waliopo kituoni kwa kupulizia dawa za kuulia wadudu katika nyumba zao, kugawa dawa za mbu, maji, juice na biskuti na baadae wakapata chakula cha pamoja na wazee na walemavu wasiojiweza.

Akizungumzia halfa hiyo ya kufunga mwaka, Hoyce Temu alisema kumekuwepo na kusahaulika kwa makundi ya watu wasiojiweza na jinsi muda unavyokwenda wanazidi kusahaulika na jamii inayowazunguka.

Alisema yeye kama Miss Tanzania ana wajibu wa kujitoa kuwasaidia watu wa aina hiyo na amekuwa akifanya maeneo mengi kwa kujumuika nao kwa kuwapa msaada na kuwafariji kwani nao wana thamani kama binadamu wengine.

"Kadri inavyokwenda kumalizika karne ya 21 kunazidi kuongezeka kwa makundi ya wasiojiweza na mimi kama Miss Tanzania nimeamua kujitoa kwa kusaidia makundi haya kwani ni wajibu wetu na tukumbuke na sisi tunaelekea huko," alisema Hoyce.

Aidha Hoyce alitoa ushauri kwa mamiss wenzake kuwa wanatakiwa kuisaidia jamii kwa kutumia fursa walizonazo mbele ya jamii kwa kutoa misaada kwa makundi ya aina mbalimbali.

Alisema kazi ya kusaidia jamii siyo ya serikali pekee na wao kama mamiss na watu wenye uwezo kwa ujumla wana wajibu wa kusaidia na sio kutazama mijini pekee kutokana na kundi kubwa la wasiojiweza kuwa vijijini.

"Sio swala la serikali pekee ... ukichaguliwa kuwa mrembo unakuwa na malengo ambayo umeyaweka hivyo watumie umaarufu, sura zao na sauti kufikia watu wa aina mbalimbali ambao wanahitaji msaada, " Na sio wazee pekee, 65% ya nchi yetu ni vijana na 20% wanajihusisha na kutumia madawa ya aina mbalimbali hivyo wanaweza kuwatembelea na kutoa elimu juu ya athari za utumiaji wa madawa hayo," alisema Hoyce.


Mdau Matukio Chuma na Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith wakifurahi jambo wakati walipowasili kwenye kituo cha Nunge.

Nae Mkurugenzi wa Lino International Agency, ambayo ndiyo waandaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga alimtaja Hoyce kama Miss bora kuwahi kutokea tangu walipoanzisha shindano la Miss Tanzania mwaka 1994.

Alisema mamiss wengi wamekuwa wakiisaidia jamii lakini Hoyce amekuwa akijitoa zaidi kuliko wengine na kufanya shindano hilo kuonekana kuwa na faida mbele ya jamii.

"Naomba niseme ukweli Hoyce anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa haijawahi kutokea miss aliyejitoa kusaidia jamii kama yeye na wapo wengine wanasaidia ila Hoyce amekuwa mstari wa mbele kwa hilo tunampongeza na tunamwomba azidi kuwa hivyo," alisema Lundenga.

Kwa upande wa Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi amemshukuru Hoyce kwa upendo amekuwa nao kwa kituo hicho ambacho awali aliwahi kukitembelea 2006 akiwa na marehemu Amina Chifupa na kumtaka kuzidi kuwa na moyo huo kwa jamii inayomzunguka.

Mgedzi pia alizungumzia changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uzio hivyo kutokuwa na hali ya usalama, kuvamiwa kwa eneo hilo na wananchi ambalo lina hekali 50.8 na tayari asilimia 50 imevamiwa na tayari taarifa ipo wizarani na wanashughulikia na zingine ndogo ndogo Hoyce akiahidi kuwasaidia.

Nae mmoja wa washiriki aliyeongozana na Hoyce, Tausi Mwenda alisema kuwa amejifunza mambo mengi kupitia halfa hiyo aliyoifanya Hoyce na kuwashauri watu wa aina mbalimbali kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia jamii kama anavyofanya Hoyce.


Baadhi ya wadau waliombatana na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (hayupo pichani) akiwemo Bi. Tausi Mwenda Mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda, (katikati) wakifurahi jambo walipowasili kwenye kituo cha Nunge, makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.


Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimkumbatia rafiki yake wa siku nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.


Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiendelea kufurahi na rafiki yake wa siku nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.


Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akitazama jicho la upande wa kulia linalomsumbua mzee Mganga Shija (66), ambaye aliomba kusaidiwa matibabu CCBRT wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.


Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi (kushoto) akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kituo hicho kwa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu aliyeambatana na Kamati ya Miss Tanzania kwenye ziara hiyo.


Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo na Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi.


Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiserebuka na mmoja wa wazee wanaoishi kwenye makazi ya Nunge kituoni hapo.


Bi. Edith (kulia) ambaye ni Dada wa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiteta jambo Bi. Tausi Mwenda mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda kabla ya kuelekea kwenye zoezi la upigaji wa dawa.


Baadhi ya nyumbani za makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.


Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda (kushoto) wakichanganya dawa ya kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa katika nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.






Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.










Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akizungumza na mmoja wa wazee (jina lake halikupatikana) kabla ya kumpigia dawa ya kuua wadudu nyumbani kwake wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.


Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith akishiriki kuondoa vyakula vyombo ili kuruhusu zoezi la upigaji wa dawa ya kuulia wadudu kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.


Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akigawa chakula kwa watoto katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza iliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.Kwa matukio zaidi bofya hapa


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...