Skip to main content

Wateja wa Tigo Pesa kuvuna 4.4bn/- gawio la robo mwaka



Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao Tigo, Obedi Laiser akielezea kuhusu gawio la mwaka huu kwa watumiaji wa Tigo Pesa, kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha



Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu gawio la mwaka huu la tigo pesa katika mkutano uliofanyika mapema leo katika makao makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es salaam.





Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao Tigo, Obedi Laiser akijibu maswali ya waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu gawio la mwaka huu kwa watumiaji wa Tigo Pesa, kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha






Dar es Salaam, Januari 13, 2016- Kampuni inayongoza katika kuleta maisha ya kidijitali kwa jamii, Tigo, imetangaza tena malipo ya robo mwaka ya shilingi bilioni 4.4 (dola milioni 2.1) kwa watumiaji wake wa huduma ya Tigo Pesa wapatao milioni 4.6.
 
“Gawio hili la faida linalipwa kwa watumiaji wote wa Tigo Pesa wakiwemo wateja binafsi, mawakala wa rejareja na washirika wetu wa kibiashara, kila mmoja kutokana na thamani ya fedha aliyojiwekea katika akaunti yake ya Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao, Obedi Laiser.
 
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Laiser amesema kuwa hii itakuwa ni mara ya kwanza Tigo kuwalipa gawio la faida watumiaji wa Tigo Pesa kwa mwaka wa 2016 akibainisha kuwa malipo hayo ni faida inayopatikana kutokana na amana ya mfuko wa Tigo Pesa uliyowekezwa katika benki za kibiashara hapa nchini.
 
“Tunayo furaha kubwa kutangaza gawio hili la faida kwa mara ya saba mfululizo tangu tulivyoanza kufanya hivi mwaka 2014. Bila shaka hii inaonyesha ni jinsi gani Tigo inajizatiti kuwaletea watanzania maisha bora ya malipo kwa njia ya mtandao,” amesema Laiser.
 
Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza duniani kutoa gawio kwa wateja wake mwaka 2014
 
“Tunaamini gawio hili la kwanza la faida ya Tigo Pesa kwa mwaka 2016 litakuwa ni kivutio kikubwa kwa mamilioni ya watumiaji wa Tigo Pesa katika kufanikisha mahitaji yao mbalimbali ya kifedha ya mwanzo wa mwaka,” amesema Laiser. 
Malipo haya kwa watumiaji wa Tigo Pesa hutolewa kwa mujibu wa mwongozo wa Benki Kuu uliotolewa mnamo Februari mwaka 2014. Mpaka sasa Tigo imelipa jumla ya 35.5bn/- kwa wateja wake tangu kuanzishwa kwa utaratibu huu mwaka juzi na kampuni hiyo.

















Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...