Skip to main content

Daily Bread Life Ministries Tanzania watoa msaada kwa waanga wa mafuriko Pawaga





Mchungaji wa Daily Bread Life Ministries Tanzania (DBL), Neema Mpeli Mwaisumbe  (kulia) akikabidhi msaada wa madogoro 15, mablanketi 10 and mashuka 10kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza kwa ajili ya waathirika wa mafuriko huko Pawaga. (Picha na Friday Simbaya)


Mchungaji wa Daily Bread Life Ministries Tanzania (DBL), Neema Mpeli Mwaisumbe ambaye aliongozana na mratibu wake Mchungaji Pawde Scout Mwasanje wamekabidhi msaada wa magodoro 15,  mablanketi 10 na mashuka 10 wenye thamani ya laki saba na sabini (770,000/-)leo kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko wa Pawaga na Mbolimboli, Iringa Vijijini.

Shirika la hilo la kidini la Daily Bread Life ambalo linaongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Mchungaji Mpeli Mwashumbe limekabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa niaba ya waathirika wa mafuriko wa Pawaga na Mbolimboli, Iringa Vijijini mkoani Iringa.


Shirika hilo pia lina kituo cha kulelea watoto yatima cha Daily Bread Life Children's Home chenye  watoto  40 kilichoanzishwa mwaka 2005 kupitia Daily Bread Life Ministries ambacho kipo Mkimbizi Iringa mjini.

Hivi karibuni WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga, wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa. 

Misaada hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko ambayo yalibomoa zaidi ya nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha Kisanga na kuwaacha wananchi wake bila makazi. 

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kasanga ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko na kuwapa pole wananchi hao (Jumatatu, Februari 22, 2016), Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote waliojitolea kuwachangia watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela hivi karibuni inaonesha jumla ya kaya 145 zilizoathiriwa na mafuriko hayo kwa makazi yao kuharibiwa zinahitaji msaada ili kurudi katika maisha yao ya kawaida.




Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...