Skip to main content

fastjet yapunguza safari za Kilimanjaro - Nairobi




Dar es Salaam, Februari 17, 2016 - Fastjet imepunguza mtiririko wa safari zake  kwenye njia ya Kilimanjaro Tanzania na Nairobi Kenya kuanzia Jumatatu Februari 15, 2016.

Fastjet ambao awali walikuwa wanatoa safari za kila siku kwenye njia hii hivi sasa watakuwa wanafanya safari kutoka Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mara mbili kwa wiki siku za Ijumaa na Jumapili tu.

Mabadiliko ya mtiririko wa safari utazifanya ndege za fastjet kuondoka Nairobi kila Ijumaa na Jumapili saa 5.40 na kutua Kilimanajaro saa 6.40 na safari ya kurudi ndege itaondoka Kilimanjaro saa 7.10 na kutua Nairobi saa 8.10.

Kupunguzwa kwa safari hizo kumetokana na kuwepo kwa mahitaji kidogo miongoni mwa wateja nyakati za wiki kutoka masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi na hivyo kufanya safari za ndege za kila siku kutokuwa nzuri kibiashara kwenye siku hizo.

Shirika hilo limesema kuwa lengo lake ni kurejesha safari hizo kwenye njia ya Kilimanjaro –Nairobi pindi tu wateja wake watakapohitaji.

Safari za kila siku za kutoka Dar es Salaam na Kilimanjaro hadi Nairobi zilianza Januari 11, 2016.

Mahitaji ya abiria kwa safari za ndege kwenye njia kubwa ya kibiashara kati ya majiji ya Dar es Salaam na Nairobi ambayo kwa
pamoja yana idadi ya watu zaidi ya milioni nane yamekuwa ni ya kuridhisha na fastjet iko kwenye mawazo kuwa ndege moja ni lazima iongezeke kwenye safari kati ya majiji haya miwili katika siku za usoni.

Matokeo ya safari za fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es Salaam yamekuwa ni makubwa ambako kunaelezwa na ukweli kuwa nauli zinazotolewa na mashirika ya ushindani kati ya nchi hizo mbili zimeshuka kwa kiwango cha hadi asilimia 40 tangu fastjet waanze safari zake.

Nauli za fastjet kwa kiwango kikubwa zipo chini kuliko zile zinazotozwa na mashirika mengine kwa safari za moja kwa moja kati ya Nairobi/Dar es Salaam  ambapo nauli zinaanzia dola 80 kwa safari moja.

Nauli hizo hazijumuishi kodi ya serikali ambayo ni dola 49 kuondokea Tanzania na dola 40 kuondokea Kenya na hivyo fastjet kupendekeza wateja wake kufanya maandalizi mapema ili kutumia fursa hiyo ya tozo la nauli nafuu.

Hata hivyo fastjet inasisitiza kuwa kupunguza safari kwenye njia kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa ya kuongeza uwezo kwenye njia za kikanda zilizopo na hali kadhalika uwezekano wa kuzindua njia nyingine mpya ya kikanda katika siku za karibuni.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...