Skip to main content

MWANAHARAKATI KHADIJA LIGANGA ANUIA KUKUSANYA PEDI KWA AJILI YA MABINTI WANAOSOMA




Kutokana na Wasichana wengi walio Mashuleni kulazimika kukosa Masomo yao katika Kipindi cha hedhi, Mwanaharakati wa Kutetea haki za Wanawake na Wasichana nchini Khadija Liganga, amelazimika kuanzisha kampeni ya kukusanya pedi 3,000 ndani ya mwezi huu ili kuwasaidia wahitaji.

Akizungumza jana katika Kipindi cha Passion Break Fast kinachorushwa na Radio Passion Fm ya Jijini Mwanza, Liganga alibainisha kwamba ameamua kukusanya pedi hizo kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuziwasilisha katika Shule 10 za Msingi na Sekondari zilizo katika Mikoa ya Mwanza na Mara hii ikiwa ni maalumu kwa ajili ya wasichana wanafunzi ambao hawana uwezo wa kumudu kununua pedi hizo.

“Tarehe Moja mwezi wa Kwanza mwaka huu, wanawake tulikutana Jijini Mwanza chini ya mpango tuliouita Women Round Table kwa ajili ya kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo kwa mwaka huu 2016. Moja ya mikakati niliyoipanga ni pamoja kuanzisha mradi uitwao Binti Box ambao umelenga kusaidia uchangiaji na upatikanaji wa pedi kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji mashuleni pamoja na kuwapa elimu ya namna ya kujiweka katika hali ya usafi wawapo katika kipindi cha hedhi”.

Alisema Liganga na kuongeza kuwa mpango huo utakuwa endelevu.

Kumekuwepo na tatizo la wanafunzi wasichana katika maeneo mbalimbali nchini kukosa masomo yao katika kipindi cha hedhi huku baadhi yao wakilazimika kuacha shule kutokana na aibu wanayokumbana nayo wawapo shuleni hii ikiwa ni kutokana na kukosa elimu ya kutosha pindi waingiapo katika kipindi cha hedhi.

Unaweza kuungana na mwanaharaki huyo kwa kuchangia pedi ambapo anapatikana kwa nambari 0713 093 801 hiyo ikiwa ni kwa wale walio mbali na Jijini Mwanza ama waweza kutembelea ofisi
za Dida Vitenge Wear zilizopo Nganza Sekondari barabara ya kwenda Chuo Kikuu cha SAUT jirani na ghorofa upande wa kushoto hapo. Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...