Skip to main content

Tigo yawapa wateja wake huduma ya WhatsApp bure



Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jana Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam 


Wafanyakazi wa Tigo na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifurahia jambo wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam



Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.



Ni kama wanasema 'tumependeza sana ngoja tujipige picha' wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam



Wageni waaalikwa wakiwa katika maski za " Emojis " wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam



Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.



Washereheshaji katika uzinduzi huo,Mc Taji Liundi na Mc Abby wakitoa maelezo jinsi gani wateja wa Tigo watakavyofurahia huduma ya whatsapp bure 


Burudani ikiendelea kutoka kwa wasanii wa kikundi maalum cha maonesho ya jukwaa wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.


Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa na viongozi wenzake kutoka tigo katika maski za "Emojis " wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam



Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washereheshaji MC Taji Liundi na MC Abby wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam


Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) Meneja wa gharama wa Tigo Jakhangic Tulaganov na Meneja masoko Olivier prentout wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency 


Bloggers wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas Muhuvile 'Joti' wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency





Dar es Salaam, Februari 2, 2016- Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa ofa ya bure ya mtandao huo wa jamii nchini.

Akitangaza upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa Tigo wanaotumia vifurushi vya intaneti vya kampuni hiyo kwa wiki na mwezi watapata huduma ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.

Huduma ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe kwa njia ya simu, ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania na duniani inatumiwa na watu wapatao milioni 900.

WhatsApp inawezesha watumiaji kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.

“Kuanzia sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia WhatsApp BURE.

Hili linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wetu inaonesha jinsi tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.

Kwa Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja wa Tigo ni kuwa na kifurushi cha intaneti cha wiki au mwezi ambacho anaweza kukipata kupitia *148*00# à Tigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki au Mwezi + WHATSAPP YA BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60. 

WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo
iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...