Skip to main content

UN CLUBS TANZANIA NA PROF. NDALICHAKO WATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA KURASINI


Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kulia) akimkabidhi msaada kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto Bi. Jack Omary(kushoto) ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii kituo cha taifa cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kurasini, hafla hii imefanyika katika siku ya wapendanao. Misaada hyo imetolewa na vijana wa UN Clubs Tanzania Network kwa kanda ya Dar es salaam pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).




UN Clubs Tanzania Network kanda ya Dar es Salaam wakishirikiana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wametoa msaada kwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Kurasini kwenye siku ya wapendanao ili kuonesha upendo mkubwa kwa watoto hao.

Vijana hao wa UN Club Tanzania Network wanafanya kazi siku ya wapendanao nchi nzima za kusaidia jamii na vijana wa jijini Dar es salaam wameungana na watoto wa kituo cha Kurasini kwa kutoa msaada na wanafunzi hao wametoka katika shule za sekondari za Zanaki, Azania, Benjamin na Jangwani.

Akizungumzia msaada huo, Afisa Ustawi wa Jamii katika kituo hicho. Jack Omary aliwashukuru kwa kuwatembelea siku ya wapendanao maana kuna watu wengine wanaitumia siku ya wapendanao kwenye starehe na hata kutumia pesa bila kuangalia kuna watu wanahitaji msaada. 

Nae Stella kutoka UN Clubs Tanzania amesema lengo la kuja katika kituo cha watoto yatima cha Kurasini nikujumuika na hao watoto ambao hawana wazazi na pia watoto wenye shida mbalimbali.




Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto) akiwakabidhi misaada watoto wa Kituo cha Kurasini, katikati ni mtoto Aboubakary Seif ambaye alipokea kwa niaba ya watoto wenzake.








Alisema inabidi kuwakumbuka hasa kwenye siku kama za wapendanao kwani kuna watu wanatumia pesa nyingi kwenye starehe kuliko kutoa misaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu hasa wazee,walemavu na hata watoto yatima.

Mtoto Aboubakary Seif anayelelewa katika kituo hicho cha Kurasini amewashukuru UN Clubs Tanzania Network Pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kwa kuwaona kama watu katika jamii wanakubalika hasa kwenye siku ya wapendanao.



Mwenyekiti wa Jangwani Fema, Jeniffer Kayombo (kushoto) pamoja na Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo wakiwakabidhi zawadi watoto wa kituo cha Kurasini jana ikiwa ni siku ya wapendanao.


Amesema wao wamesijsikia furaha kutembelewa na vijana wenzao na kuwapa moyo hasa kwa kusoma kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Pia aliwaomba watu wengine wenye uwezo waje kutoa msaada maana matatizo ni mengi na matatizo hayo yatatatuliwa kwa misaada ya wadau mbalimbali.



Zuwena (kushoto) akimkabidhi mpira mtoto aliyewawakilisha wenzake kituoni hapo.

Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza jambo mbele ya watoto (hawapo pichani) walipowatembelea watoto hao wenye mahitaji maalumu kwenye kituo cha Kurasini, jijini Dar es Salaam katika siku ya wapendanao.

Mwenyekiti wa Jangwani Fema, Jeniffer Kayombo akiwaasa watoto kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.


Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akiwagawia watoto hao soda pamoja na biskuti ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako pamoja na vijana wa UN Clubs Tanzania Network kwa kanda ya Dar es salaam walitoa zawadi hizo.


Baadhi ya vijana wa UN Clubs Tanzania Network kwa kanda ya Dar es salaam kutoka katika shule za Sekondari za Jangwani, Zanaki, Benjamini na Azania wakiwagawia zawadi watoto wenye mahitaji maalumu.



Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Kurasini.

Hii ndio misaada iliyotolewa katika kituo cha kululea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam.




Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akiwa kwenye picha ya pamoja na Umoja wa vijana wa youth advisory board (FEMA YAB) walipotembelea watoto yatima katika kituo cha Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akiwa kweye picha ya pamoja na watoto wa kituoni hapo.





Picha ya pamoja. 




Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...