Skip to main content

WAZIRI UMMY AWAGEUKIA VIONGOZI NA KAZI YA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU

Viongozi wote kuanzia ngazi ya vijiji hadi mkoa wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu hadi kufikia Machi, 30 mwaka huu.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na kikosi kazi cha udhibiti wa ugonjwa wa kipindupindu, kulia nina Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt.Nassoro Mzee.

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokutana na kikosi kazi cha cha udhibiti wa kipindupindu mkoani Dodoma

"Kipindupindu siyo suala ya afya peke yake, bali ni suala mtambuka hivyo sekta zote zinapaswa kujumuika katika kupambana na kutokomezwa ugonjwa huu.

Ummy alisema kipindupindu bado ni changamoto na janga hivyo kila mkoa unatakiwa kuliwekea kipaumbele kwakuwa ugonjwa huo unaua kwa haraka hivyo viongozi wote washiriki kikamilifu na si kuwaachia waganga wakuu wa mikoa au wilaya.

Aidha alisema licha ya kuwa na sheria ndogo za kila halmashauri za kusimamia usafi na mazingira lakini katika kudhibiti kuenea kwa kipindupindu lazima litakuja suala la kufungia biashara hususani za mbogamboga, matunda pamoja na chakula.

"Suala la kukusanya mapato lipo na litaendelea kuwepo lakini suala la kipindupindu linapoteza maisha,maisha hayatafutwi lakini pesa zinatafutwa lakini ukikosea utapoteza maisha ya watu wengi,” alisema Waziri Mwalimu.



Kaimu mganga mkuu mkoa wa Dodoma Dkt.Nassoro Mzee akisoma taarifa ya hali ya kipindupindu ya mkoa.

Ummy alisema tangu kipindupindu kiingie nchini Agosti mwaka jana, halmashauri zimetumia pesa nyingi katika kutokomeza ugonjwa huo, lakini wangeweza kuzuia mapema, pesa hizo zingeenda kutatua tatizo la madawati katika shule za msingi nchini.

"Mnapoona hamjaridhika na uendeshaji wa migahawa, msisite kuzifungia mara moja, mapato mtakusanya haraka kwa kuwa na nguvu za pamoja baada ya kutokomeza ugonjwa na kuweza kuingiza mapato mengi na kwa haraka tofauti na kuwa na hilo tatizo,” alieleza.

Hata hivyo alivitaka vikosi vyote vya mikoa nchi, kuwashirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa dini zote kuweza kuelimisha kuweza kutoa elimu ya jinsi gani ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa waumini wao.

Mkoa wa Dodoma umetumia takribani Shilingi Milioni 124 toka kipindupindu kimeingia mkoani humo na hadi leo kuna wagonjwa wanne katika kambi ya kipindupindu wilaya ya Bahi, jumla ya wagonjwa 450 waliugua na vifo12, wilaya zilizoathirika ni Bahi, Dodoma mjini na Chamwino.



Baadhi ya kikosi hicho toka idara na wadau mbalimbali wakimsikiliza Waziri huyo.

Mtaalamu toka Wizarani Dkt. Vida Makundi (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwenye kambi hiyo.

Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Bahi, Dkt. Gerald Maro akielezea jambo, kikosi kazi toka Wizara ya Afya na wale wa mkoa (hawapo pichani) mara baada ya kufika kwenye kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye zahanati ya Isangha iliyopo wilayani Bahi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Isangha,Andrea Lusinde(katikati) akielezea jinsi kijiji hicho kilivyoweza kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na kipindupindu pamoja na ujenzi wa vyoo na kuvitumia, jumla ya vyoo zaidi ya 300 vimejengwa katika kaya,Kulia ni diwani wa kata ya Chibelela, Chalula Gerald


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...