Skip to main content

WILAYA YA CHUNYA KUTUMIA ZAIDI YA BILLIONI 35

CHUNYA: MADIWANI na viongozi wa vijiji wilayani Chunya katika Mkoa Mpya wa Songwe,wametakiwa kusimamia na kulinda Sheria za misitu ili kuweza kupunguza tatizo la uvamizi wa maliasili hiyo mhimu unaofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu.

Hayo yalisemwa Mwishoni mwa Wiki na Mkuu wa wWlaya hiyo, Elias Tarimo, wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ambapo alisema kuwa haiwezekani wavamizi wa misitu wanavuna misitu mpaka kufikia hatua ya kuhatarisha uwepo wake wakati viongozi hao wanaangalia.

Aliwaagiza madiwani pamoja na viongozi wengine wa vijiji kuwa walinzi kwa kuanzia katika maeneo yao kabla ya wavamizi hawajakamatwa na uongozi wa Wilaya kwa madai kuwa hali hiyo inapunguza hali ya uwajibikaji.

Alisema inatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kuzuia vituo vilivyo wekwa vya kuzuia mazao hayo kupitisha, na wale ambayo wamekuwa ni wazembe kwa kushindwa kuzuia katika vizuizi wafukuzwe na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

“Inasikitisha misitu inaharibiwa kwa kiasi kikubwa wakati madiwani na viongozi wa vijiji mkiwa mpo katika maeneo hayo, hamuwezi kuwa na kisingizio cha kwamba hamuwaoni maana mpaka viongozi wa Wilaya wanakuja kuwakamata wahalifu kwenye maeneo yenu pamoja na kuwa wanakuwa ni wageni, hivvyo nawaagiza kuwa walinzi wa misitu hiyo na sitarajii uhalifu huo kuendelea,” alisema Tarimo

Aliwataka wananchi wa wilaya hiyo hasa wale wa vijijini kusaidia Serikali katika kutoa taarifa juu ya waharifu hao wa misitu ili kuweza kuwadhibiti kwa madai kuwa endapo misitu hiyo itakwisha madhara yatawakumba wao.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Chunya, Bosco Mwanginde, alisema pamoja na kupitisha bajeti hiyo mapato ya ndani yakikusanywa kiuhakika kwa kuanza kuzuia wezi wa mazao ya mistu mapato yataongezeka zaidi.

Alisema kumekuwepo na tabia ya kuvuna Mbao na kupitishwa usiku hali ambayo ni wizi wa kuiibia Halmashauri mapato, ambapo aliwambia madiwani kusaidia kuinua mapato ya halmashauri kwa kuzunguka maeneo yote ambayo mazao ya misitu yanavunwa ili wenye vibali vya kufanya shughuli hiyo walipe ushuru na wasio navyo wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Akisoma mapendekezo ya bajeti hiyo katika kikao cha baraza la madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Sophia Kumbuli, alisema bajeti hiyo imependekezwa kwa lengo la kuiinua wilaya hiyo.

Kumbuli alisema katika bajeti hiyo wamependekeza kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 35.9 na kwamba matumizi ya kawaida na Mishahara watatumia shilingi Bilioni 24.4 miradi ya Maendeleo bilioni 7.8 na matumizi mengineyo Bilioni 3.6.

Alisema kiasi cha shilingi bilioni 1.1 zitakuwa kwa ajili ya maendeleo ngazi ya wilaya na vijijini, mpango wa kilimo wilaya milioni 179, program ya maji (RWSSP) kiasi cha milioni 899.9, mpango wa maendeleo ya Elimu milioni 566.3 na miradi mingineyo.

Madiwani walisema bajeti hiyo imelenga kukamilisha miradi ya barabara, maji, kilimo, mpango wa kuendeleza mfuko wa ngozi, ukarabati wa soko, ujenzi wa jengo jipya la utawala, afya, ikiwa ni pamoja na kuendeleza shughuri za wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...