Skip to main content

RC MBEYA, AMOS MAKALA, ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WATUMISHI WA SERIKALI



*Kila Alhamisi wakuu wa Wilaya, wakuu wa idara kwenda vijijini




Na Gordon Kalulunga, Mbeya

MKUU wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala, amekabidhiwa rasmi ofisi yake leo na aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Abbas Kandoro, huku akitoa maagizo manne mazito kwa watumishi wa serikali.


Makala alisema kuwa, wakuu wote wa wilaya na wakuu wa idara katika Halmashauri za wilaya zilizopo mkoa wa Mbeya, kila siku ya Alhamisi kuanzia saa nne mpaka saa nane mchana ni marufuku kukaa ofisini bali wanatakiwa kwenda kupokea kero za wananchi vijijini na kuzishughulikia.


“Mimi sijaja kutengua torati bali kutimiliza. Kila mmoja wetu atimize wajibu wake na kuacha vyeo vya uadmin wa magroup kwenye Whats App na face book” alisema Makala.


Alisema agizo lingine hataki kusikia masuala ya ugonjwa wa kipindupindu katika Halmashauri za mkoa wa Mbeya, huku akiagiza kuwa lazima mazingira yawekwe safi.


Kuhusu watumishi hewa wanaolipwa mishahara alisema jambo hilo halihitaji digrii ili kuelewa na kulitekeleza ndani ya siku 15 kama lilivyo agizo la Rais Dkt. John Magufuli, hivyo Wakurugenzi na maafisa utumishi wameagizwa kuwabaini haraka.


“Nimekabidhiwa taarifa hapa na Mkuu wa mkoa mstaafu kaka yangu Abbas Kandoro, najua kuna taarifa za upungufu wa madawati katika wilaya zetu, hivyo basi kila Mkurugenzi wa wilaya akaandike barua kuthibitisha alichopeleka kwenye taarifa yake na wala msidanganye na kuogopa kueleza ukweli ili wakati wanataka kunishughulikia mimi barua zenu ziwe ushahidi kuwa mlidanganya” alisema Mkuu huyo wa mkoa.


Aliwaeleza kuwa yeye kwa umri wake siyo mtu wa kukaa ofisini na kauli mbiu yake ni kwamba walipo wananchi, palipo na kero naye yupo na kwa sasa chini ya serikali ya awamu ya tano wanacheza mchezo uitwao usiniguse.


Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Abbas Kandoro, alisema kuwa anawashukuru sana marais wote wa Tanzania kwa kufanya kazi nao na sasa anastaafu akiwa na miaka 66 ambapo ametumikia taifa hili kwa miaka 40.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...