Skip to main content

“Mwanamke wa Afrika bado anakabiliwa na changamoto” - Waziri Ummy Mwalimu



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Mkutano huu wa wiki mbili unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.

Wakati mamia ya wanawake kutoka serikalini na Asasi za Kiraia wakiwa wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao unaojadili hali yao katika maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake hususani wale wa Afrika wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha nyuma kimaendeleo.

Ni wanawake hao wanaoishi katika nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha, wenye kukabiliwa na uhaba na ukosefu mkubwa wa chakula, maji safi na salama, matatizo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ndio ambao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya ushirikiano ili malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030) yaweze kuwafikia.

Waziri Mwalimu ametoa wito huo jana jumatatu, wakati alipotoa hutuba kwa niaba ya nchi za Afrika katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya wanawake (CSW) ambao umeanza hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akitoa hotuba katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). 

Changamoto hizo pamoja na nyinginezo nyingi zikiwamo kutopata fursa ya huduma za afya ya uzazi salama, elimu na usawa wa kijinsia zinamfanya mwanamke wa Afrika ashindwe kushindana na wanawake wenzie hususani wale walioko katika mataifa yaliyoendelea. 

Waziri Mwalimu ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu wa wiki mbili, alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya nchi za Afrika kutokana na kwamba Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika kwa mwezi huu wa March.

Amewaeleza washiriki wa mkutano huo waliofurika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwamba ingawa pamekuwapo na makubaliano na mapendekezo mengi kuanzia yale yaliyofikiwa huko Beijing, bado mwanamke anayeishi katika nchi zenye migogoro na vita barani Afrika ataendelea kuachwa nyuma na hivyo kukosa fursa ya kushinda na wenzie.

“ Ingawa vita, ukame wa kutisha, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, ukichanganya na ukosefu wa fursa za kiuchumi, kijamii na kisiasa ni matatizo yanayowakabili watu maskini lakini mwanamke ndiye anayeathirika zaidi,” alieleza Waziri Mwalimu.

Na kuongeza kwamba Afrika inaendelea kutilia mkazo hoja ya kuwashirikisha wanawake katika majadiliano na utoaji wa maamuzi katika masuala yanayowagusa yakiwamo masuala yanayohusu mabadiliano ya tabia nchi na usuluhishi wa migogoro. 

Alieleza kwamba, nchi zinazoendelea na zilizoendelea zinapashwa kuongeza kasi ya ushirikiano na ubia baina yao ili kufanikisha utekelezaji wa Agenda 2030), Makubaliano juu Mabadiliko ya Tabia nchi yaliyofikiwa huko Paris Ufaransa mwaka jana na makubaliano yaliyofikiwa na waafrika wenye kupitia Ajenda 2063 , ili katika umoja wake dunia basi iweze kumwondoa mwanamke na jamii nzima kutoka hapa ilipo na kufikia hali bora zaidi ya maisha.

Kama hiyo haitoshi Waziri alisema, Afrika inaamini pia katika uwezeshwaji wa Sekta binafsi, kupanua wigo wa ujasiliamali kama njia mojawapo ya kukuza uchumi endelevu , usawa wa kijamii, usawa wa jinsia, ulinzi wa mazingira na uwezeshaji wa mwanamke. 

Mada kuu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake, ni “Uwezeshaji wa Wanawake na uhusiano wake na Ajenda 2030.

Awali akizungumza mwanzoni mwa mkutano huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amasema tangu alipoingia madarakani mwaka 2006 amejjitadi kuongeza nafasi za viongozi wanawake katika Idara za Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwa katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manong.

Akitilia msisitizo hoja na haja ya kupanua wigo wa wanawake kushika nafasi katika ngazi za juu za maamumizi, Ban Ki Moon amesema, ingawa nchi nyingi zimejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi bado kuna Nchi Tano ambazo hazina wanawake katika Mabunge yao ili hali Nchi nyingine 7 hazina mawaziri wanawake katika serikali zao.

Naye Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw Monges Lykketoft, akizungumza wakati wa mkutano huo, pamoja na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Agenda 2030 ambayo ameitaja kuwa ni jumuishi ameendelea kupigia chapuo la kutaka Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa awe Mwanamke.

Na Mwandishi Maalum, New York


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...