Skip to main content

AZANIA BENKI YASHEREHEKEA SIKU YA MAMA KWA KUGAWA DAWA NA VIFAA VYA USAFI HOSPITALI YA AMANA


Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kulia), kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, akimkabidhi kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Francis Yango (kushoto), dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.milioni 5 vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Dar es Salaam leo asubuhi. Wapili kulia ni Muuguzi wa zamu,Getrude Massawe na Antusa Lasway.

Wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa mbele ya vifaa na dawa walivyotoa msaada kwa Hospitali hiyo.
Hapa ni furaha tupu kabla ya kukabidhi msaada huo.




Mwonekano wa maboksi yenye msaada huo baada ya kupokelewa.
Vifaa hivyo vikipelekwa kwa walengwa.
Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kushoto), akimkabidhi dawa za meno na sabuni, Judith Kimei katika wodi ya wazazi. Kulia ni Muuguzi wa zamu Antusa Lasway.

Ofisa wa benki hiyo, Neema Tumsifu akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.
Ofisa wa benki hiyo, Valentina Chesama akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.

Wafanyakazi hao wa Bebki ya Azania wakiondoka Hospitalini hapo baada ya kukabidhi msaada huo.




BENKI ya Azania imetoa msaada wa dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 5 katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Ilala Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo wakati wa kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara, Mwanahiba Mzee alisema kila mara benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii kulingana na ratiba yao ambapo mwaka huu waliona ni vema msaada huo waupeleke Hospitali hiyo.

Alisema mwaka katika kusherehekea sikukuu ya wanawake waliona ni vema kutoa msaada hasa katika wodi ya wajawazito ukizingia kuwa sikukuu hiyo inawahusu.

"Tumetoa msaada wa dawa mbalimbali kama dettol, spiritis, mabomba ya sindano, micoprostol, vitamini k na nyingine nyingi pamoja na vifaa vya usafi kama vile mifagio, sabuni na dawa za mswaki" alisema Mzee.

Kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali hiyo, Francis Yango akizungumza wakati wa kupokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mkuu, Shadrack Shimwela aliishukuru benki hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia.


"Tunawashukuru sana Azania Bank Ltd kwa msaada wenu lakini tunawaomba muende mbele zaidi kama mtaweza mtujengee walau wodi ambayo itaingiza walau vitanda 30 na wodi hiyo muandike jina la benki yenu kwani changamoto kubwa tulionayo kwa sasa licha ya kuwa na vitanda vya kutosha tuna uhaba wa wodi" alisema Yango.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...