Skip to main content

HATIMAYE CHAMA CHA ADC CHAFANYA MKUTANO MKUU,MSAJILI AWAMWAGIA PONGEZI


Waziri wa kilimo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar amnbaye ni mlezi wa chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE -ADC nchini Tanzania Mh HAMAD RASHID akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika Jijini Dar es salaam leo(Picha na EXAUD MTEI)

Baada ya chama cha ALIANCE FOR DEMOCTARIC CHANGE –ADC kuingia katika migogoro ya kiuongozi ndani ya chama hicho siku za hivi karibuni Hatimaye hali ya Amani imerejea ambapo chama hicho leo kimeingia katika mkutano mkuu uliowakutanisha wajumbe mbalimbali kutoka kila kona ya nchi.


Katika mkutano ambao umehudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo waziri wa kilimo wa serikali ya Zanzibar ambaye alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho ambaye pia ndiye mlezi wa chama Mh HAMAD Rashid,viongozi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na wajumbe mbalimbali wa chama hicho.
Makamu mwenyekiti wa ADC Mama ADELA STOLIC akihutubia wakati akifungua mkutano huo Mkuu mapema leo

Akizngumza wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo HAMAD RASHID amesema kuwa chama cha ADC ni chama ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia watanzania,kikiwa na itikadi zake,sera zake na mipango yake hivyo hakipo tayari kufwata sera za chama kingine chochote nchini na swala la kushiriki chaguzi mbalimbali ni moja kati ya sera zao hivyo hawapo tayari kususia uchaguzi wa aina yoyote kwani ndio njia pekee ya kupata viongozi wa nchi.
Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini A SISTY LEORNAD NYAHOZI akitoa hotuba fupi kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa nchini 

Ameleza kuwa chama chake kimeanza mipango kabambe ya kujiimarisha Zaidi kwa lengo la kuwaletea mabadiliko ya kweli watanzania baada ya wapinzani wao waliokuwa wakiongoza serikali iliyopita na sasa hawapo kushindwa kufanya hivyo kwa miaka yote iliyopita hivyo amewataka watanzania kuanza kukiamini chama cha ADC kwani ndio dira pekee ya mabadiliko kwa watanzania kwa sasa.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa viongozi wa chama hicho mara baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama kiongozi huyo amewataka wanachama wa chama hicho wakae tayari kwa kuwa siku yoyote chama kitaitisha uchaguzi wa kupata viongozi wapya.

Naye msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini Mh SISTY LEORNAD NYAHOZI akizungumza katika mkutano huo amekipongeza chama hicho kwa kukubali kuingia katika uchaguzi wa marudio Visiwani Zanzibar ambapo walishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 3 jambo ambalo amesema ni ukomavu wa kisiasa kwa chama kichanga kama hicho kushiriki uchaguzi mkubwa kama ule na kupata mafanikio hayo.

Aidha amesema kuwa chama hicho kimeonyesha ukomavu Zaidi baada ya kutokea mtafaruku na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho na kufanikiwa kulimaliza kidemocrasia jambo ambalo amesema linafaa kuigwa na vyama vingine vya siasa nchini.
Chama hicho kilijikuta katika migogoro iliyosababisha hadi kutimuliwa kwa aliyekuwa mwenyekiti wake SAID MIRAAJ kwa kile kiliichoitwa kukiuka matakwa katiba ya chama ambapo ilielezwa kuwa mwenyekiti huyo alipinga kitendo cha viongozi wa chama kuingia katika uchaguzi wa Zanzibar wa marudio jambo ambalo alilipinga na kusababisha mtafaruku baina yake na aliyekuwa mgombea wa chama hicho visiwani Zanzibar ambaye kwa sasa ni waziri HAMAD RASHID

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...