Skip to main content

MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WAMZIKA KINYAMBE



























Msanii Ringo



Kitale



msanii wa vituko show






Mke wa Msanii Kinyambe (katikati)





MBEYA: MAMIA ya wakazi ya jiji la Mbeya wamzika aliyekuwa msanii wa vichekesho James Petro Nsemwa (30) maarufu kama Kinyambe ambaye alifariki dunia jumatano mkoani Mbeya, katika makaburi ya Hayombo Uyole Igawilo mkoani Mbeya. 


Msururu wa wakazi wa jiji la Mbeya pamoja na magari ulitembea kutoka nyumbani kwa wazazi eneo la makondeko mtaa wa mtakuja kata ya Igawilo kuelekea makaburi ya bonde la uyole kwa umbali kilometa tatu na nusu. 


Pia baadhi ya wasanii kutoka Dar es Salaam wakiongozwa na kitale waliudhuria mazishi ya msanii mwenzao ingawa hapakuwepo na uwakilishi wa viongozi ngazi ya mkoa uliyofika mazishini . 


Msiba huo uliosimamisha shughuli mbalimbali kwa muda ili kupisha msururu wa watu na magari ambao ulikuwa ukielekea makaburini yaliyopo eneo la Nsalaga. 


Baba wa marehemu, mzee Lugendelo Nsemwa, ameiambia SIMBAYABLOG akiwa nyumbani kwake Uyole, kuwa mwanaye ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa uchekeshaji, alianza kuumwa tangu Juni mwaka jana, ambapo moyo, tumbo na miguu ilikuwa imejaa maji pamoja na pafu la kushoto. 


Alisema tatizo hilo lilipelekea mapafu yake kushindwa kufanya kazi sawasawa. 


“Kwa kipindi kirefu alikuwa amelazwa katika hospitali mbalimbali kama vile Uyole, Ifisi, Rufaa na hospitali ya mkoa wa mbeya, hali yake ilibadilika, alizidiwa na kupoteza fahamu, na bahati mbaya Jumatano saa 3 usiku akafariki dunia,” alisema mzazi huyo. 


Komediani huyo aliyetamba kwa kubadilisha sura na sauti yake katika filamu za uchekeshaji nchini, James Petro Nsemwa a.k.a Kinyembealizaliwa tarehe 19.09.1985 katika kijiji cha Mahanji- Matamba. 


Kinyambe hakuwa na kiwango kikubwa cha elimu ambapo aliishia kidato cha pili mwaka 1999, kisha akajiunga na masomo ya sanaa katika mkoa wa Tanga kwa mwaka miwili. 


Marehemu alikuwa msanii wa kuigiza na kuchekesha ambaye alizunguka mikoa karibu yote yaTanzania na nchi za nje kama vile Malawi, Msumbuji na Zambia. 


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...