Skip to main content

YANGA YAFIKISHA POINTI 71 TASLIMU, BAADA YAKUIUA MBEYA CITY 2-0 SOKOINE

Mbuyi Twite akitolewa nje  baada ya kuumia



Mashabiki wa Yanga Sc wakishangilia ngoli ya Vincent Bossou


Golikipa wa Mbeya City Juma Kaseja akipapangua goli,


Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari cha Yanga na Msemaji wa klabu hiyo, Yanga Jerry Muro akiongea wanahabari baada ya mechi kati ya Yanga Vs Mbeya FC kumalizika ambapo Dar Young Africans iliibuka mshindi wa magoli mawili kwa bila.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari cha Yanga na Msemaji wa klabu hiyo, Yanga Jerry Muro (kulia) akiwa na Meneja wa Simbayablog Friday Simbaya.


Amissi Tambwe amefunga boa lake la 21 leo, akimfunga kipa mkongwe nchini Juma Kaseja.


Tambwe raia wa Burundi amefunga bao hilo likiwa ni la pili kwa Yanga katika mechi ambayo wameshinda kwa mabai 2-0 dhidi ya Mbeya City.


Bao lake hilo la 21 msimu huu ni gumzo, sasa anamuacha mshambuliaji Mganda wa Simba, Amissi Kiiza kwa mabao mawili kwa kuwa ana 19.


Tambwe amefunga bao hilo akiwa umbali wa takribani mita 23, ilikuwa kama anatuliza lakini tayari alijua Kaseja alikuwa amesogea mbele, akaachia shuti lililojaa wavuni moja kwa moja.

GOOOOOOO Dk 15, Bossou anaunganisha mpira wa kichwa wa krosi ya Abdul na kuandika bao kwa Yanga. Kwa udhamini wa Maji Africa




MBEYA: YANGA imezidi kuupendezesha ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City jioni ya jana Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Yanga sasa inafikisha pointi 71, baada ya kucheza mechi 28 na ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Ndanda FC na Majimaji kukamilisha msimu.

Hadi mapumziko, tayari Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na beki Mtogo, Vincent Bossou.

Bossou alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 15, akimalizia krosi ya beki mwenzake, Juma Abdul kutoka kulia aliyeanzishiwa kona fupi na winga Simon Msuva.


Amissi Tambwe akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la pili


Hata hivyo, Yanga ilipoteza wachezaji wake wawili kipindi cha kwanza, mfungaji wa bao Bossou na kiungo Mkongo Mbuyu Twite ambao wote waliumia.

Nafasi ya Twite ilichukuliwa na Salum Telela dakika ya nane na Kevin Yondan alichukua nafasi ya Bossou dakika ya 29.


Kwa ujumla Yanga ilitawala mchezo kipindi cha kwanza na ingeweza kuondoka inaongoza kwa mabao zaidi kama si kosakosa za wazi mbili tatu.

Kipindi cha pili, nyota ya wana Jangwani iliendelea kung’ara na kuzidi kuwafunika wenyeji Mbeya City uwanjani.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe akafunga bao lake la 21 katika Ligi Kuu msimu huu kuipatia Yanga bao la pili dakika ya 85 kwa shuti la nje kla 18.

Mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma hakuwa mwenye bahati kutokana na kukosa mabao mawili ya wazi, moja kila kipindi wakati Simon Msuva alipoteza nafasi moja nzuri kipindi cha pili. 

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya.

Mbeya City; Juma Kaseja, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Tumba Swedi, Haruna Shamte, Kenny Ally, Suleiman Mangoma/Hamidu Mohamed dk66, Ramadhani Chombo ‘Redondo/Raphael Alpha dk46, Salvatory Nkulula, Geoffrey Mlawa na Joseph Mahundi/Ditram Nchimbi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...