Skip to main content

Serikali yaipongeza SBL kwa uhifadhi wa mazingira





Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais mazingira Mh. Luhaga Mpina akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Bi Helene Weesie wakati wa ziara yake leo katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Chang’ombe Dar es Salaam alipowasili kiwandani hapo kujionea namna kampuni hiyo inavyofanya shuguli zake kwa kuzingatia sera za utunzaji wa mazingira.












Mheshimiwa Luhaga Mpina Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais mazingira akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Bi Helene Weesie wakati wa ziara yake leo katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo Chang’ombe Dar es Salaam alipowasili kiwandani hapo kujionea namna kampuni hiyo inavyofanya shuguli zake kwa kuzingatia sera za utunzaji wa mazingira.

















Mheshimiwa Luhaga Mpina Naibu waziri ofisi ya makamu wa raisi mazingira (katikati) akiongozana na Mhe. Mbunge wa Temeke , Abdallah Mtolela (kushoto) na Meneja wa mradi wa kusafirisha maji taka wa kampuni ya bia ya Serengeti Bwana Peter Mkongwa wakiongozana kuelekea kwenye mtambo wa kusafirisha majitaka kiwandani hapo.




Meneja wa mradi wa kusafirisha majitaka wa kampuni ya bia ya Serengeti Bwana Peter Mkongwa akielezea namna mradi huo unavyofanya kazi wakati wa ziara ya Mhe. Luhaga Mpina Naibu waziri ofisi ya makamu wa raisi mazingira alipotembelea kuona mtambo wa kusafirisha majitaka unavyofanya kazi kiwandani hapo mapema



Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti, John Wanyancha akifafanua jambo wakati ya ziara ya Mhe. Luhaga Mpina Naibu waziri ofisi ya makamu wa raisi mazingira alipotembelea kuona ujenzi wa mtambo wa kusafirisha majitaka kiwandani hapo pamoja na namna kiwanda kinavyofanya shughuli zake kwa kuzingatia sera za mazingira.




DAR ES SALAAM, Julai 14, 2016: Kampuni ya bia ya Serengeti leo imepongezwa na serikali kwa juhudi zake za uhifadhi wa mazingira na kutajwa kuwa mfano mzuri wa mashirika binafsi yanayoounga mkono jitihada za kulinda mazingira nchini.




Haya yamesemwa leo na naibu waziri katika ofisi ya makamu wa rais, anayeshughulika masuala ya mazingira na muungano, Luhaga Mpina, alipofanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha SBL kilichoko Chang’ombe jijini Dar es Salaam.


Katika ziara hiyo naibu waziri alijionea harakati mbalimbali zinazofanywa na SBL katika uhifadhi wa mazingira ikiwemo ujenzi wa bomba maalum lenye urefu wa kilomita 2.1 linalosafirisa majitaka kutoka kiwandani hapo hadi mfumo wa majitaka wa DAWASCO ulioko kurasini.


“Napenda kuipongeza sana kampuni ya SBL kwa ujenzi wa bomba hili la majitaka ambalo tunaamini litasaidia katika kuendeleza kuimarisha usafi na uhifadhi wa mazingira katika kiwanda hiki na pia kwa jamii inayokizinguka.


Mpina aliongozana na mbunge wa Temeke Abdalla Mtolea, ujumbe kutoka Baraza la Mazingira (NEMC) na uongozi wa juu wa halmashuri ya wilaya ya Temeke.


Akitolea ufafanuzi ujenzi wa mfumo huo wa majitaka, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha amesema kampuni hiyo imetumia zaidi ya shilingi 470 kukamilisha mradi huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya SBL ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira.


“Bomba hili la usafirishaji wa majitaka ni kielelezo cha jinsi ambavyo SBL inajali na kulinda mazingiar kwa manufaa mapana ya jamii yetu na ustawi wan chi ya Tanzania,” alisema Wanyancha akisema kwamba majitaka yanayosafirishwa na bomba husafishwa kwanza kiwandani kabla ya kuelekezwa kwenda kwenye mfumo wa majitaka wa DAWASCO.




Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...