Skip to main content

AGRA yashawishi matumizi ya teknolojia kuongeza tija katika kilimo


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wadau mbalimbali wa kilimo walipowasiri katika maonesho ya wakulima ya nanenane katika viwanja vya John Mwakangale jijijni Mbeya na baadaye kufunga maonesho hayo. (Picha na Friday Simbaya)


. Kwa miaka 10 imetumia dola za Marekani milioni 51 kuendeleza kilimo




MBEYA: TAASISI ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA) imetoa wito kuwapo kwa matumizi zaidi ya teknolojia kwa wakulima wadogo ili kuwa na uhakika na usalama wa chakula huku wakiingiza ziada katika soko.



Mtendaji wa taasisi hiyo nchini Tanzania Dk Mary Mgonja alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya wakulima ya nanenane katika viwanja vya John Mwakangale mjini hapa.



Katika mkutano huo taasisi zinazoshirikiana na AGRA katika kuleta mabadiliko kwa wakulima zipatazo 10 zilikuwapo.


Dk Mgonja alisema ana matumaini makubwa na hali ya baadae ya kilimo nchini Tanzania na kuongeza kwamba matumizi zaidi ya teknolojia ndio njia pekee ya kuwainua mamilioni ya wakulima wadogo kutoka katika lindi la umaskini.


“Tanzania kuanzia mwaka 2006 imekuwa ikipewa kipaumbele na AGRA na kwamba miradi 96 imepewa ruzuku inayofikia dola za Marekani milioni 51,” alisema.


Kwa mujibu wa Dk Mgonja ruzuku hizo zimetoa mchango mkubwa katika kukabiliana na changamoto za wakulima wadogo katika mnyoror wa thamani wa shughuli zao kuanzia masuala ya mbegu, udongo, soko, sera hadi fedha.


Sehemu ya uwekezaji huo imezaa matunda kwa kupata aina tofauti za mbegu zilizoboreshwa kukabiliana na hali za maeneo; matumizi sahihi ya mbolea; utunzaji baada ya mavuno; teknolojia ya hifadhi za nafaka na ubunifu wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuinua kilimo.


“Ninatoa wito kwa wakulima kukumbatia njia mpya za teknolojia katika kilimo ili kupata tija zaidi ;kuanzia matumizi ya mbegu bora zilizoboreshwa mashambani hadi kwenye matumizi ya teknolojia mpya ya kuhifadhi mavuno; Njia hizo kama zitatumika vyema zitaongeza uzalishaji na kupunguza upotevu wa mavuno. Mambo hayo ni muhimu ili wakulima wadogo wajinasue kiuchumi,” alisema Dk Mgonja.


Tangu kuingizwa kwa teknolojia ya mifuko maalumu ya kuhifadhi nafaka na bidhaa jamii ya mikunde, kampuni tatu zinashughulika na kutengeneza hifadhi hizo, huku zikiuzwa na kuwafikia mamia kwa maelfu ya wakulima.


Aidha Dk Mgonja aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kupiga hatua kwenye kuboresha sera ya kilimo yenye lengo la kukabiliana na changamoto za wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo.


“AGRA itaendelea kushirikiana na wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi kuhakikisha kwamba shughuli za AGRA nchini zinakwenda sambamba na juhudi za serikali ya Tanzania katika kuboresha kilimo,” alisema Dk Mgonja.

Aidha aliongeza kwamba mchango mkubwa wa AGRA umekuwepo katika Matokeo Makubwa sasa na Kilimo Kwanza 


Alisema taasisi ambazo zilisaidiana na AGRA kuleta mapinduzi ya kilimo katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ni pamoja na Tanzania Seeds Trade Association (TASTA), CSDI, Equity Bank, Unyiha Associates, BRITEN, RUDI, AGROZ. Nyingine ambazo zilikuwa ni taasisi za umma ni pamoja na ARI Uyole, Chollima AGRO, ARI Mlingano na kituo cha SAGCOT .

Dondoo za Shuhuda

Kwa muda AGRA imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba kunakuwa na mazingira mazuri ya biashara ya mbegu kupitia mradi wa Micro Reforms for African Agribusiness (MIRA) : Mradi huu ulizaa matunda mema kwani kuanzia Juni 2016, kumekuwepo na sera mpya ya mbegu.


Mkurugenzi Mtendaji Tanzania Seeds Trade Association (TASTA), Bw. Baldwin Shuma. Alieleza kufurahishwa na Sera hiyo ilitengenezwa kwa namna pekee ambapo inaruhusu sasa makampuni ya mbegu kuzalisha mbegu ambazo zilifanyiwa utafiti na taasisi za umma.

Naye Dk Matilda Kalumuna, wa Taasisi ya utafiti wa kilimo ya Mlingano –Tanga, amesema kwamba AGRA imesaidia taasisi yake kwa kuipa ruzuku ya dola za Marekani 400,000 kusaidia kuimarisha mifumo yake ya kuangalia ubora wa mbolea.


“Kupitia mradi huu taasisi ilifundisha wakaguzi wa mbolea 100; wachambuzi 15 wauzaji pembejeo wenye uelewa 338 na wadau 8000.

Kutokana na mradi huo makampuni mbalimbali na wauzaji wa pembejeo za kilimo waliamua kwa hiari yao kujisajiri na TFRA;mbolea iliyoko sokoni inasajiliwa, kukaguliwa na kuchambuliwa kwa lengo la kuona mbolea zisizokidhi viwango zinajulikana na kuondolewa sokoni.


“Benki ya Equity Tanzania imeingia ubia na AGRA kuanzisha mfuko ambao utasaidia kununuliwa kwa vifaa vya hifadhi ya nafaka. Katika mradi wa majaribio Njombe, Morogoro na Iringa, tutatoa mikopo ya sh kuanzia milioni 5 hadi 30 ili kununua mifuko maalumu ya kuhifadhia nafaka; vihenge vya chuma na vifukofuko (cocoons), kuanzia mwezi huu,“ alisema Mkuu wa biashara ya kilimo wa benki ya Equity, Enesto Josephat

Mtaalamu wa viazi mviringo Owekisha Kwigizile, kutoka kituo cha utafiti wa viazi cha SAGCOT katika mazungumzo yake alisema: “hapa nchini Tanzania tuna aina tatu viazi mviringo zinazotambuliwa kisheria pamoja na kwamba viazi mviringo ni chakula kikuu nchini. SAGCOT na wadau wengine wa AGRA tunafanya juhudi kuongeza vipando bora zaidi ambavyo vitatoa tija kubwa na kuongeza mavuno”

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...