Skip to main content

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI HUU LEO,SOMA HAPO KUJUA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo September 09 2016 amemteua Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.



Aidha Rais Magufuli amemteua Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu. Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.






NA KAROLI VINSENT
VYAMA vya wafanyakazi nchini pamoja na Asasi za kiraia nchini ambayo ipo chini ya mwamvuli wa mtandao wa watetezi wa Haki za Bindamu nchini (THRDC) Wamelitaka bunge la Jamhuri wa muungano wa Tanzania kutopitisha mswaada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii unaokwenda kuzuia fao la kujitoa,

Hivyo basi wamesema endapo wabunge wakikaidi na kuupitisha mswaada huo na baadae kuwa sheria basi wafanyakazi nchini watagoma ikiwemo kwenda mahakamani kupinga mswaada huo pamoja na kujitoa kwenye mifuko yote ya hifadhi ya jamii kutokana na mswaada huo kumkandamiza mfanyakazi nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam kwa wakati mmoja, na viongozi tofauti wa vyama vya hivyo,ambao ni Gratius Mkoba ambaye ni Rais wa Chama cha wafanyakzi nchini (TUCTA) na pia ni Rais wa chama cha walimu nchini (CWT),Nicomemas Kajungu ambaye ni Katibu mkuu wa Chama cha wafanyakzi wa kwenye migodi nchini na nisharti (NUMET),Bi Majura ambaye ni Katibu mkuu wa chama cha wafanyakzi wa viwandani nchini (TUICO) huku wakiwakilishwa na Onesmo Olenguruma ambaye ametoka (THRDC).

Mkoba amesema wamejitokeza kuupinga mswaada huo baada kujilidhisha kuwa mswaada huo ukupita bungeni na kuja kuwa sheria utakuwa unakuja kumuumiza mfanyakazi kutokana na kutopata stahiki zake anazokatwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.


Amesema kitendo cha mfanyakazi kuambiwa makato yake anayokatwa kwenye mifuko hiyo ya kijamii hataruhusiwa kuichukua hadi atapofisha umri wa miaka 60, amedai kuwa jambo hilo ni hatari kwa wafanyakazi na kuzidisha uonevu kwa kwao .

"Tunawaomba wabunge walioangalie hili,ni vigumu sana kuingia kichwani kama leo hii tumefikia hatua ya kutaka mtu anayeacha kazi akiwa na miaka 25 au 30,akae hadi kufikia miaka 60 ndipo achukue poesa zake sawa na yule aliyefanya kazi kwa kipindi cha miaka 60 na kustaafu,hapa inaonekana wameshindwa kuelewa dhana dhima matumuzi ya pesheni,kwani lengo lake ni kumsaidia yule anbapofanya kazi ili maisha yaendelee"amesema Mkoba.

Mkoba amesema Mswaada huu utazidi kuwaumiza hata wafanyakazi wa sekta binafsi ambao wengi wao wamekuwa wanafanya kazi kwa mikataba ya miaka miwili au mitatu akidai kuwa mkataba wake ukiishi kwa kipindi hicho kumfanya asubili hati afike miaka 60 ndio akachukue fedha yake ni kukandamiza na kumnyima fursa.

"Yaani lazima tusimame na tupinge hili kwani watu wengi wanapoaacha kazi wanatumia fedha kujianzisha miradi yao ya maendeleo na kujikimu lakini leo unamvyomtaka achukue akiwa na umri wa miaka 60 ni kumyima fursa,hata wanafunzi wanapomaliza vyuo upenda kujiunga na kazi ya mikataba ili wanamaliza mikataba yao hutumia fedha za mifuko ya jamii kujiendeleza kimasomo"ameeongeza kusema Mkoba.

Kwa upande wake Bi Majura naye amesema hata TUICO Wamesikitishwa na hatua ya serikali kuupeleka mswaada huo kimya kimya bila hata kuwashirikisha wadau wa sekta ya ajira huku akidai kuwa mswaada huo umekuwa na usiri mkubwa jambo analodai linawatia shaka.

Kwa upande wake Kajungu amesema Mswaada huo unatawaumiza hata wafanyakazi wa migodi amabo wengi wao wanafanya kazi kwa mikataba kwani wanaomiliki migodi upewa mikataba ya miaka michache hivyo inawalazimu kuwaajiri wachimbaji migodi wa kwa mkataba hivyo kitendo cha kuwepo kwa sheria hiyo kutawaumiza wafanyakazi wa migodi.

Hata hivyo,Olenguruma amewataka wabunge kuondoa ikadi zao vyama na kuweka mbele maslahi ya wananchi kwa kuungana ma kuupinga mswaada huo kwani haufai kabisa.

"Tunaaamini wabunge wataungana na sisi kuzuia mswaada huo, na kama sauti zetu itapuuzwa,wafanyakazi wanaweza chukua hatua mbali mbali kwama vile kwenda mahakamani, kugoma na kujitoa kwenye mifuko ya kijamii, na waajiri wanaweza sitisha kupeleka michango kwenye mifuko hiyo na kufunga account za mafao hayo hadi hapo usalama wa fedha za wafanyakazi utakapopatikana katika mifuko ya jamii hasa suala la fao la kujitoa"amesema Olenguruma.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...