Skip to main content

WANANCHI KATA YA KITWIRU WAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UJENZI

Na Esta Malibiche

Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Msenza amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa kuwa waadilifu na kutojiingiza katika mauzo ya Ardhi ili kuepuka na Migogoro ya Ardhi.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na viongozi wa kata ya Kitwiru iliyopo Manispaa ya Iringa katika ziara yake aliyoifanya jana[leo]huku akiambatana na katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu,Watalaam wa Afya na Mazingira kutoka mkoani na Manispaa ya Iringa.

Masenza alisemakuwa lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua ujenzi holela katika Mtaa wa Kibwabwa’ B’,kukagua uchimbaji n a upondaji wa mawe unaofanywa na baadhi ya wananchi katika eneo la shule ya Msingi Mnazi mmojapamoja na Kukagua hali ya usafi wa Mazingira katika mtaa wa Kitwiru na Uyole .

"Ninatoa agizo kwa wale wote wanaoporomosha mawe na kujenga naomba wachukuliwe hatua za kinidhamu.Milimani,Mabondeni na katika vyanzo vya uhifadhi hairuhusiwi kujengwa,ninawaomba Manispaa iweke vibao vitakavyoonyesha maeneo yaliyohifadhiwa ili yasivamiwe na kuuzwa,"alisema Masenza.

Aliwasihi wananchi kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kupata vibari vya ujenzi na mara wanapotaka kununua uwajanja na kujenga nyumba ili kuepukana na Migogoro ya udanganyifu kutoka kwa viongozi wasio waaminifu.

"Wenyeviti wa mitaa tuendelee kutoruhusu wananchi wasitende makosa ya kujenga bila kufuata kanuni na taratibu za ujenzi ikiwa ni pamoja na kufuata michoro iliyopo," alisema Masenza

Awali kaimu Mkurungenzi wa Manispaa ya Iringa Omary Mkangama, akisoma Taarufa ya kuzuia ujenzi holela,Mikakati ya kulasimisha makazi,kuzuwia uvamizi katika maeneo ya milimani na uasafi wa Mazingira kwa mkuu wa mkoa wa Iringa, alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni miongoni mwa Halmashauri zinazokuwa kwa kasi kubwa hivyo kupelekea tatizo la ujenzi holela kukithiri katika maeneo yasiyopimwa na uvamizi katika maeneo ya mlimani.

Mkangama alisema hali hiyo inatokana na ongezeko la idadi ya watu,kutanuka kwa mji na ufinyu wa maeneo yaliyopimwa. Pia maeneo yaliyokithiri kwa ujenzi holela ndani ya Manispaa hiyo ni pamoja na Ipogolo, Mapogolo, Ndiuka, Semtema, Mtwivila, Mwangata, Mlandege, Igumbilo, Kihondombi, Isoka, Mafifi na milima ya Mkimbizi.

"Mikakati mbalimbali tumeiweka ili kuzuwia ujenzi holela na uvamizi wa maeneo yasiyopimwa ikiwa ni pamoja na kutumia makampuni ya wapima binafsi kupima viwanja kwenye maeneo yenye michoro ya mipango miji kwa gharama zilizotolewa na Serikali.

Alisema wanaendelea kutoa vibali vya ujenzi kwa haraka hasa kwenye maeneo yaliyopimwa ili kuepuka wananchi kujenga pasipo kufuata taratibu.Kuendelea kuuza viwanja vilivyopimwa kwa kuzingatia pato la mwananchi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Kitwiru Simba Nyunza akisoma Taarifa ya mikakati ya uboreshaji wa matumizi ya vyoo bora na Usafi wa mazingira kwa ujumla alisema kuwa majengo 2255 ndiyo yenye vyoo bora sawa na asilimia 93 ya majengo yote yaliyotambuliwa.

Nyunza alisema kuwa mikakati ya kata ni kuondoa na kuwezesha idadi ya majengo 168 yenye vyoo vinavyohitajika kuboreshwa viboreshwe mpaka kufikia mwisho wa mwezi Novemba mwa huu 2016.Na kwa wale watakaobainika kushindwa kutekeleza agizo hilo sheria ndogo ya Halmshauri itatumika.

"Baadhi ya wakzi wanashindwa kujenga vyoo bora kwa kuwa maeneo yao yana Ardhi oevu,hivyo wanashindwa kuchimba mashimo kwa kuwa maji chini ya Ardhi yapo jirani sana. Pia Ardhi iliyopo ni ya mchanga sana. Hivyo tunashirikisha wataalamu wa ziada kutoka ofisi ya Afya ya Manispaa kutoa Elimu ya Ujenzi wa vyoo bora katika maeneo oevu,"alisema Nyunza

Akielezea mikakati ya kutdhibiti ujenzi holela alisema ili kudhibiti ujenzi holela, kamati za mitaa ambazo ni kamati za mazingira ambazo ziliagizwa kufuatilia vibali vya ujenzi na kutoa maelezo ya namna ya kuomba vibari vya ujenzi kwa wajenzi wote kila mtaa ujenzi unapotokea.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...