Skip to main content

JUMIA TRAVEL YATOA TUZO KWA HOTELI ZINAZOFANYA VIZURI NCHINI TANZANIA




Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee (kushoto), akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.



Hafla ikiendelea.



Wadau wakiwa kwenye hafla hiyo.



Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee (kulia), akimkabidhi tuzo Flora Rwehumbiza katika hafla hiyo.



Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee akimkabidhi tuzo ya Ushirikiano Mkubwa mwaka 2016 kwa Meneja wa Huduma za Hoteli ya Amaan Bungalows, Daudi Fundi (kushoto). Hafla ya sherehe hizo zilifanyika jana katika ukumbi wa Mayfair jijini Dar es Salaam.



Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee (kulia) akikabidhi tuzo ya Mshirika Bora Katika Biashara mwaka 2016 kwa Mtendaji wa Mauzo wa Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam, Emma Sizya. 





Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee (kushoto), akizungumza na wanahabari.

MTANDAO unaoongoza kwa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika wa Jumia Travel umetoa tuzo kwa hoteli na washirika wake wakati wa hafla fupi iliyofanyika siku ya Alhamisi katika ukumbi wa hoteli ya Mayfair jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika Dar es Salaa jana, Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania Fatema Dharsee alibainisha kuwa tuzo hizo zimelenga kuleta chachu katika matumizi ya huduma za hoteli mtandaoni nchini na kupanua wigo wa huduma kwa wateja.


“Leo hii tumejumuika hapa kuzitambua na kuzitunuku hoteli zinazotoa huduma nzuri pamoja na kupendwa na wateja wa ndani na nje ya nchi. Mbali na sababu hizo lakini kikubwa zaidi ni kwa hoteli hizi kuendana na mabadiliko ya teknolojia kupitia mtandao wa intaneti ambao unawezesha huduma zao kufikiwa na mtu yeyote duniani,” alisema Dharsee.


“Hoteli zote zilizojiunga au kujumuishwa kwenye mtandao wetu wa ‘Extranet’ zinazo fursa kubwa za kuongeza ufanisi na thamani ya biashara yao kwani hazitegemei tena wateja wanaokwenda moja kwa moja kutafuta huduma kwenye meza zao za maulizo. Kupitia mtandao wetu ambao unapatikana kwenye kompyuta, tabiti na simu, unamwezesha meneja wa hoteli au mapokezi mahali popote walipo mbali na vituo vyao vya kazi kupokea maombi ya wateja kisha kuthibitisha au kubatilisha upatikanaji wa huduma husika,” aliongezea Dharsee

Aliendelea mbele kwa kufafanua zaidi kuwa vipengele vya tuzo za Jumia Travel Tanzania vilivyokuwa vikiwaniwa ni pamoja na:

Chaguo la Wasafiri – hii ilitolewa kutokana na maoni ya wateja au wageni wengi walioitembelea; Hoteli Iliyoonesha Ushirikiano Mkubwa – hii ilitolewa kwa kigezo cha kuthamini mchango na ushirikiano wake; Hoteli Bora Inayochipukia – hii ilitolewa kutokana na juhudi na jitihada zilizooneshwa katika sekta nzima kwa ujumla; Hoteli Iliyopokea Maombi Zaidi Kutoka Kwa Wateja – hii ilitolewa kwa mujibu wa kuwa na maombi mengi kutoka kwa wateja; na Mshirika Bora Katika Biashara – hii ilitolewa kwa kutuunga mkono na mchango mkubwa katika biashara.

“Ningependa kutoa shukrani za dhati kwa hoteli zote zilizokubali wito na kuhudhuria hafla hii. Uwepo wenu hapa jioni ya leo unaonyesha kutuamini na kuunga mkono jitihada za kuinua sekta ya utalii na ukarimu nchini hususani kuhamasisha kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani,” alihitimisha Meneja Mkaazi huyo wa Jumia Travel nchini Tanzania.

Katika hafla hiyo hoteli zilizojinyakulia tuzo hizo ni pamoja na Serena ambayo ilitunukiwa tuzo ya Mshirika Bora Katika Biashara; Tanzanite Executive Suites ilitunukiwa tuzo ya Chaguo Bora la Wasafiri; Amaan Bungalows ilitunukiwa tuzo ya Hoteli Iliyoonesha Ushirikiano Mkubwa; Harbour View Suites ilitunukiwa tuzo ya Hoteli Iliyopokea Maombi Zaidi Kutoka Kwa Wateja; na Slipway ambayo yenyewe ilitunukiwa tuzo ya Hoteli Bora Inayochipukia.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo Mtendaji wa Mauzo kutoka Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam Emma Sizya amesema kuwa amefarijika kupokea tuzo hiyo na kuipongeza kampuni ya Jumia Travel Tanzania kwa kuja na kitu hiki cha kipekee.

“Kwanza ningependa kuipongeza Jumia Travel Tanzania kwa kuja ni hizi tuzo ambazo ninaamini kuwa zitaleta mchango mkubwa katika kuhamasisha sekta ya hoteli nchini. 

Tumekuwa tukiona sekta mbalimbali zikiwa na tuzo zao lakini yetu ikiwa imelala kidogo, huu ni mwanzo mzuri na ninaamini waandaaji hawataishia hapa,” alisema na kumalizia Sizya kwamba, “Serena siku zote tunajivunia kuwa mbele katika kuunga mkono jitihada za wadau mbalimbali wanaofanya kazi na sisi. 

Lengo letu kubwa ni kuona kuwa kwa pamoja tunashirikiana katika kuwashawishi wateja kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ambapo sasa hivi kupitia kampuni kama hii unaweza kupata huduma zetu mtandaoni.”


Hafla hiyo imeambatana na kuadhimisha miaka mitatu tangu Jumia Travel kuanzishwa pamoja na kampeni maarufu ya mauzo inayoendelea kwa jina la ‘Black Friday’ ambayo imeanza Novemba 14 mpaka Novemba 25, 2016. 

Matarajio ya kampuni kwa wiki hizi mbili za mbili ni makubwa ambapo imelenga kuwapatia wateja fursa ya kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma za awali kwa ajili ya msimu wa sikukuu kwa gharama nafuu. 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...