Skip to main content

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AVIFUTIA USAJILI WA KUDUMU VYAMA VITATU VYA SIASA




Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Monica Mnanka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha msajili wa vyama kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Msaji Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza na Msajili wa Vyama, Jaji Francis Mutungi.



Msajili wa VVyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kufutwa kwa usajili wa kudumu wa vyama vitatu vya siasa ambavyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) na Chama cha Jahazi Asilia. Kulia ni Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza.



Mkutano na wanahabari ukiendelea.


Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.




Na Dotto Mwaibale


MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992, amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kuanzia leo hii.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi Jaji Mutungi alivitaja Vyama alivyovifuta kuwa ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), kilichopata usajili wake Novemba 15, 2001 kilichokuwa kikiongozwa na James Mapalala kama Mwenyekiti wa Taifa na Mwaka Lameck Mgimwa kama Katibu Mkuu.


Chama kingine alichokifutia usajili wa kudumu ni Chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) kilichopata usajili Machi 4, 2003 kilichokuwa kikiongozwa na Peter Kuga Mziray kama Rais Mtendaji Taifa na Nziamwe Samwel kama Katibu Mkuu.


Jaji Mutungi alikita chama kingine alichokifuta kuwa ni Chama cha Jahazi Asilia kilichokuwa kikiongozwa Kasimu Bakari Ally kama Mwenyekiti wa Taifa na Mtumweni Jabir Seif kama Katibu Mkuu ambacho kilipata usajili wa kudumu Novemba 17, 2004.


Mutungi alisema vyama hivyo vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambapo kila chama klipewa taarifa ya nia ya Msajili wa Vyama vya siasa kufuta usajili wake wa kudumu na kutakiwa kueleza kwanini kisifutwe ambapo vilishindwa kutoa sababu za kuridhisha kuwa havikukiuka sheria na bado vinavyo sifa za usajili wa kudumu.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...