Skip to main content

UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KAZI ZA CCM




Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo, Dar es Salaam leo asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).



Mkutano ukiendelea.



Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.



Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.



Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana (kushoto), akizungumza na wajumbe hao.



Madabida akiwakaribisha wajumbe hao.



Karibuni wajumbe kutoka China.







Na Dotto Mwaibale


UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa chama hicho, Jia Bo.

Madabida alisema ziara ya ujumbe huo hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa Taifa hilo Hayati Mao Tse-Tung.

Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili nchini kufuatia ziara ya baadhi ya makada wa CCM walipokwenda nchini China ambapo walijifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.

Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho kutoka China ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

" Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi nyingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba, Ulaya hasa katika siasa za kijamaa" alisema Chana.

Alisema wenzetu wa China wapo karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao hapa nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyonayo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...