Skip to main content

WASANII KUTOKA NIGERIA KUNOGESHA FAINALI YA TAMASHA LA FIESTA 2016




Msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade (kushoto) , akisalimiana na msanii Snura Mushi alipokuwa amewasili ukumbi wa mikutano wa Kampuni ya Simu ya Tigo kuzungumza na wanahabari wakati akijitambulisha kwao Dar es Salaam leo jioni, kuhusu uwepo wake kwenye hitimisho la Tamasha la Fiesta litakalofanyika kesho viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.



Mratibu wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga (kulia), akizungumza wakati wa kuwatambulisha wasanii wa hapa nchini na kutoka Nigeria ambao watatoa burudani kesho katika viwanja vya Leaders.



Msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade (kulia) , akizungumza katika mkutano wa kujitambulisha kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo jioni, kuhusu uwepo wake kwenye hitimisho la Tamasha la Fiesta litakalofanyika kesho viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msanii mwenzake, Tecnomile na katikati ni msanii Snura Mushi.



Msanii Tecnomile (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Meneja Huduma wa Masoko wa Tigo, Olivier Prentout.



Mkutano na wanahabari ukiendelea.



Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.



Picha zikipigwa na msanii Tecnomile.


Na Dotto Mwaibale


WASANII Yemi Alade na Tecnomile kutoka Nigeria kesho watapanda jukwaani na washindi 16 washindano la Tigo Fiesta Super Nyota katika fainali ya Tamasha la Fiesta 2016 lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.


Wasanii hao wanatarajiwa kutoa burudani na nguvu katika viwanja hivyo itakayokwenda sanjari na kumpata mshindi wa tamasha hilo kwa mwaka 2016.


Akizungumza katika mkutano wa kujitambulisha kwa wanahabari msanii Tecnomile alisema Tanzania kwake ni kama nyumbani na Diamond na Vanesa ni washikaji zake hivyo atatoa burudani kali ili washikaji wakumbuke ujio wake.


Kwa upande wake msanii Yemi ameshukuru mapokezi makubwa yaliyofanywa dhidi yao na kuwa anaipenda Tanzania na anajisikia yupo nyumbani na pia anakipenda Kiswahili.


Yemi alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hasa wapenzi wa muziki kufika kwa wingi katika viwanja hivyo kupata burudani la kukata na shoka.


Wasanii wa hapa nyumbani ambao ni washindi Super Nyota 16 watakaopanda jukwaani kumsaka bingwa wa Tamasha la 

Fiesta 2016 ni Nchama Anton a.k.aNchama, Raphael Charles 

Manengoa.k.a Manengo kutoka (Mwanza), Ibrahim Jumaa.k.a Mpanduji(Shinyanga) , Obed Moses a.k.a O strings (Muleba),

Salum Asmana.k.a Alinacha ( Kahama), Gasper Festoa.k.a YOW (Tabora) Alex Joseph .a.k.a TIZO ( Singida), Godfrey Andrew Mhojaa.k.a NEXUS( Dodoma) Hamad Hussein a.k.a Med Botion (Morogoro) Cyril Henry Isidora.k.a So Real(Tanga) Wilson Pascal a.k.a Willy Desmiller( Mtwara ) Charles Marikia.k.aGerere (Moshi) Mohammedy Amiry a.k.a Croozy (Arusha), AminaChibabaa Ammy Chiba (Mbeya) 

Leonard John Haulea.k.asauti classic (Sumbawanga).


Tamasha la Tigo Fiesta 2016 limekuwa likiendeshwa kwa ubia baina Kampuni ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania huku Tigo ikiwa ndio mdhamini mkuu.



Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...