Skip to main content

MTUMISHI WA TANAPA ADAI HAKI ZAKE KWA MWAJIRI




Aliyekuwa mtumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA), Emiliyo Mwadila Lugiriva pichani amemuomba Rais John Pombe Magufuli aingilie kati suala la madai yake ya kutelekezwa na mwajiri wake, baada ya kustaafu kwa hiari mnamo tarehe 01.07.2007. 

Akiongea na Nipashe jana mstaafu huyo alitaja baadhi ya madai yake hayo kuwa ni pango la chumba kimoja ambacho kilihifadhi mizigo iliyoletwa Iringa na kuahidiwa kusafirishwa hadi sehemu husika yaani, Minjingu, Manyara, pango la vyumba viwili ambavyo familia ilikua ikishi mjini Iringa kabla ya kupewa nyumba nyingine kwa ajili ya familia na pango la vyumba viwili ambavyo alitumia baada kutekelezwa na mwajiri wake tangu tarehe 30.10.2007. 

Alisema kuwa mnamo mwezi wa kumi (10) 2007 aliambiwa atasafirishwa hadi nyumbani kwake (Mijingu), lakini cha ajabu alifikishwa Iringa na kuambiwa hapo ndiyo nyumbani kwake, wakati nyumbani kwake ni Minjingu wilyani Babati, mkoani Manyara. 

Alitaja madai mengine kuwa ni posho ya kujikimu yeye na familia yake tangu kutekelezwa na mwajiri huyo pamoja na nauli kutoka Serengeti-Ruaha-Iringa-Tungamalenga-Msembe. 

Alisema kuwa aliomba kustaafu kwa hiari kutokana ya matatizo ya afya yake kwani, alikuwa anasumbuliwa na magonjwa ya kisukari, vidonda vya tumbo, macho na masikio. 

Lugiriva alizaliwa mwaka 1952 na mwaka 2007 akiwa na miaka 55, hivyo kutokana na maradhi hayo yalipelekea utendaji wake kudhoofu ndipo alipoandikia barua ya kustaafu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadi za Taifa (TANAPA) kuomba kustaafu kwa hiari. 

Aidha, alisema kuwa aliwahi kuwaandikia barua ya madai Ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii tarehe 31.07.2011 bila mafanikio, kwa hivyo amemuomba Rais Magufuli amsaidie katika suala lake, kwani anateseka na familia yake.
Alisema kuwa anaomba asafirishwe nyumbani kwako Mijingu wilayani babati, mkoani Manyara, kwani huko ndio alikozika wazazi wake na baadhi ndugu zake.

Alisema kuwa katika mazungumzo yake na Kaimu Mhifadhi Mkuu kupitia barua yake tarehe 03.07.2007 kuhusu haki zake, aliambiwa anastahili kupewa ‘Certificate of Service’ , malipo ya PPF (Pension) pamoja na gharama ya kusafirishwa yeye na familia yake na mizigo isiyozidi tani 1.5 hadi nyumbani kwake. 

Nipashe ilifanikwa kuongea na mmoja ya viongozi wa Hifadhi ya Taifa Ruaha na kudai kwamba madai yake (Lugiriva) wanayafahamu na kuongeza kuwa suala hilo linachanganya. 

Kiongozi huyo alidai kuwa suala la mstaafu huyo linachanganya sana kwa sababu wakati anaajiriwa alijiandikisha kuwa nyumbani kwake ni Iringa lakini baada ya kupelekwa Iringa alibadilisha mawazo kuwa kwake ni Minjingi Wilaya ya Babati, mkoani Manyara. 

Alisema kuwa bwana Lugiriva ametembea sehemu mbalimbali kuhusu suala lake ameenda mpaka mahakamani lakini bado hajaridhika na majibu yake. 

Naye Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Dk. Christopher Timbuka  akiongea kwa njia  simu alisema suala hilo kuhusiana mtumishi huyo linaeleweka na kwa sasa   lipo mikono mwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa linashughulikiwa.

Alisema kuwa masuala waliyamaliza na mkuu wa mkoa na bawana hiyo  aliapa kuwa kwao ni Iringa na sio Mijingu kama anavyodai mtumishi huyo.

Kuhusu suala la hati ya utumishi yaani certificate of service nalo alisema kuwa hilo lipo juu ya hawezi kulisemea.







Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...