Skip to main content

HIVI NDIVYO CCM ILIVYOSUKWA...



Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.


Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;-


1. Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi vikaoni.


Ili kuwa na vikao vya Chama vyenye tija imeamuliwa kama ifuatavyo:-



a). Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158 kama ifuatavyo:-


Wenyeviti wa Mikoa
Mikoa ya Bara 26x1 = 26
Mikoa ya Zanzibar 6x1 = 6


Wajumbe wa NEC wa Mikoa
Mikoa ya Bara 26x1 = 26
Mikoa ya Zanzibar 6x4 = 24
Wajumbe wa NEC wa Taifa
Kutoka Bara = 15
Kutoka Zanzibar = 15


Nafasi za Mwenyekiti = 7


Wajumbe wa NEC wa Jumuiya
UVCCM = 5
UWT = 5
WAZAZI = 5
Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni = 5


Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM = 1


Wajumbe wa NEC kutoka BLW = 3


Katibu wa Kamati ya Wawakilishi = 1


Wajumbe wa NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao
- Mwenyekiti wa CCM = 1
- Makamu Mwenyekiti (B) = 1
-Makamu Mwenyekiti (Z) = 1
- Makamu wa Rais = 1
- Waziri Mkuu = 1
- Makamu wa Pili wa Rais (Z) = 1
- Spika wa Bunge = 1
- Spika wa BLW = 1
- Mwenyekiti wa UWT = 1
- Mwenyekiti wa WAZAZI = 1
-Mwenyekiti wa UVCCM = 1
- Katibu Mkuu – WAZAZI = 1
- Katibu Mkuu – UWT = 1
- Katibu Mkuu – UVCCM = 1
Jumla: 158

#. Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vifanyike kila baada ya miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.


b). Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati Kuu wawe 24 badala ya 34 kama ifuatavyo:-


Mwenyekiti wa CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar)
Makamu wa Rais
Katibu Mkuu wa CCM
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Waziri Mkuu
Makamu wa Pili wa Rais (Z)
Spika wa Bunge la Tanzania
Spika wa BWL
Mwenyekiti wa WAZAZI
Mwenyekiti wa UWT
Mwenyekiti wa UVCCM
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania


Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar.


#. Vikao vya kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili vifanyike kila baada ya miezi minne badala ya miezi miwili isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.


c). Kwa ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa wajumbe watatu ambao ni:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa - 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Mkoa - 2


#. Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Mkoa vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.


d). Kwa upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wapunguzwe kwa kuwoandoa:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya - 1
Katibu wa Kamati ya Madiwani - 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)- 2
Jumla: 4


#.Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Wilaya vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.


#. Muundo wa Wilaya za Chama uendane na muundo wa sasa wa Serikali.


Kata,Tawi na Shina
Idadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50 hadi 300.


Idadi ya kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301 hadi 1,000.
Hata hivyo idadi hii izingatie eneo la kijiografia na wingi wa wanachama katika eneo hilo.


Vikao vya kawaida vya Kamati za Siasa za ngazi hizi viwe vinafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.


#. Nafasi za Uongozi
Mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa Chama Toleo la 2012 kifungu cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:-
Mwenyekiti wa Tawi,Kijiji au Mitaa.
Mwenyekiti wa Kata/Wadi.
Mwenyekiti wa Jimbo, Wilaya na Mkoa.
Makatibu wa Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika.
Mbunge, Mwakilishi na Diwani.


#. Viongozi wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji badala yake waongoze na kusimamia shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni.


#.Vyeo ambavyo haviko kwenye Katiba
Vyeo ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM haviruhusiwi katika Chama au Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali kama Wenyeviti wa ngazi mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k), Makamanda (UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote.


#. Uhakiki wa Wanachama wa CCM
Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wa CCM na Jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu. Uhakiki huu uendane na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki na kadi za CCM tu.


#. Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi
Jumuiya za CCM zimetakiwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za Jumuiya ziendane na matakwa ya Katiba ya CCM.


#.Uaendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya za Chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi).
Makatibu Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na Kamati Kuu na Manaibu Katibu Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.


#. Wakati tukiendelea kubaki na Bendera yenye rangi ya kijani na njano na alama ya jembe na nyundo, Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi.


#. Utumishi katika Chama na Jumuiya zake. Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za Watumishi wa Chama na Jumuiya zake.


Nafasi za Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya zitaondolewa na badala yake kazi zao zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya za Chama wa Mikoa na Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa. Utaratibu huu utakipunguzia Chama Cha Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa Chama na Jumuiya zake katika Mikoa na Wilaya.


#. Tathimini ya hali ya Kisiasa na Uchaguzi wa Zanzibar .
Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kuundwa kwa Kamati maalum ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar 2015.


# Mwenyekiti wa Kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari 2017, Mikoa na Wilaya ambazo hazijaleta taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti na Nidhamu kabla ya tarehe 30/01/2017.


#. Uhakiki wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi ukikamilika Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa mapema iwezekanavyo.


#. Maamuzi na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na Kanuni za Jumuiya za Chama.


#. Kwa mambo yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya Katiba, Mkutano Mkuu utaandaliwa mapema mwakani na kutafakari na kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba.


Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarietiambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.


#.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.
#. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi
#. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
#. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.


Imetolewa na:-


NAPE NNAUYE
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
13/12/2016

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...