Skip to main content

KAYA 6,464 WILAYANI KILOLO ZINANUFAIKA NA MPANGO WA TASAF

Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Iringa, William Kingazi akizungumza na walengwa wa malipo katika mpango wa unusuru kaya maskini Kijiji cha Magunguli wilayani Mufindi, mkoani Iringa hivi karibuni. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)



KILOLO: Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imefanikiwa kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuanzia zoezi la utambuzi, uandikishaji, uhakiki na malipo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Hayo yalisemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Kilolo, Grace Killo wakati wa mahojiano maalum na Nipashe ofisini kwake jana.

Alisema kuwa jumla ya kaya maskini 6,464 zilitambuliwa na kujengewa uwezo katika vijiji 70 vilivyo kwenye mpango.

Alisema kuwa ugawaji wa ruzuku katika vijiji 70 vilivyo kwenye mpango umesababisha kuongezeka kwa mzunguko wa fedha kwenye vijiji hivyo na kusababisha kukua kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Alisema kuwa baadhi ya kaya nufaika zimefanikiwa kuanzisha miradi midogo midogo kwa ajili ya kukuza kipato ili waweze kujitegemea hata baada ya mradi kuisha kwa mfano; ufugaji wa kuku, mbuzi na shughuli za kilimo cha mbogamboga.

“…Uhamasishaji umefanyika ili walengwa wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) hadi kufikia Novemba jumla ya Kaya 3,878 kati ya kaya 6,401 zilijiunga na mfuko wa afya ya jamii sawa na asilimia 60.6, uhamasishaji unaenedelea,” alisema Killo.

Alisema kuwa kaya maskini zilizotambuliwa na kuwezeshwa kupata huduma za afya, malezi, chakula na elimu mpaka sasa kiasi cha fedha zilizotolewa ni shilingi 1,602,245,272.72.

Afisa Maendeleo ya Jamii, Killo alisema kuwa zipo changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mpango kama vile baadhi ya Kaya kutotumia fedha kulingana na malengo ya mpango wa TASAF, kwa mfano; kutojiunga na CHF na kutoanzisha miradi midogo midogo kwa ajili ya kuongeza kipato.

Alisema kuwa baadhi ya kaya zilishindwa kusimamia mahudhurio ya shule na kliniki kwa watoto kwa asimilia 80 kama muongozo wa TASAF unavyoelekeza.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na miundo mbinu mibovu ya barabara na mawasiliano ya simu kwa baadhi ya vijiji.

Pia alisema kuwa halmashauri hiyo inapokea kiasi cha fedha kisichotosheleza kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa mpango kwa ngazi ya wilaya na vijiji ukilinganisha na hali halisi ya mahitaji.

Ili kuweza kutatua changamoto hizo halmashauri inaendelea kuzijengea uwezo Kaya nufaika juu ya utumiaji wa fedha kulingana na malengo ya mpango kwa kutumia kamati za Usimamizi za Jamii (CMCs), wawezashaji ngazi ya Wilaya (PAA Facilitators), uongozi wa kijiji kwa ujumla pamoja na kusisitiza kupeleka watoto shule na kliniki.

Hata hivyo, Afisa Maendeleo ya Jamii huyo alisema kuwa kaya 92 kati ya 6,464 zimefariki kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuzolota kiafya na kuwa na umri mkubwa kwa baadhi ya kaya.

Mwisho















Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...