Skip to main content

MADIWANI MERU WAMKATAA MKURUGENZI





makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani Meru akiwa anachangia hoja katika baraza hilo 



baadhi ya madiwani wa meru wakifuatilia kikao



mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Christopher Kazer akifafanua jambo kwa waandishi mara baada ya baraza kumalizika



mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Christopher Kazer akijibu hoja mbele ya madiwani wa meru



baadhi ya madiwani wakifuatailia






Habari picha zote na Woinde Shizza, Arusha




BARAZA la madiwani Halmashauri ya Meru mkoani Arusha wamkaanga Mkurugenzi wasema hana uwezo wa kuongoza Halmashauri hiyo.

Akitoa maazimio ya kikao cha baraza kilichokaa siku mbili kilichowajumuisha madiwani,wakuu wa idara mbalimbali na wataalam Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Willy Njau Alisema wametafakari kwa kina utendaji wa Mkurugenzi na kubaini kuwa hafai.


" Tumejadili ajenda ya utendaji usioridhisha wa Mkurugenzi wetu na tumeona kuwa haufai kutokana na mambo mengi anayoyafanya yanakiuka kanuni na taratibu za Halmashauri"alisema Njau.

Aidha Njau alisema Mkurugenzi huyo ameonekana kukata mawasiliano na mwenyekiti wa Halmashauri jambo alilosema siyo sahihi.

Alisema pia ameweza kukata mawasiliano na madiwani wa Halmashauri hiyo pamoja na kusababisha hata wakuu wa idara kutokuwa na mawasiliano na madiwani jambo linalorudisha maendeleo nyuma.

Aliongeza kuwa Mkurugenzi huyo ameshindwa kukusanya makusanyo ya pesa kiasi cha milioni 150 kilichokusudiwa kukusanywa tangu Julai hadi septemba mwaka huu jambo alilosema linaweza kusababisha Halmashauri kutopewa ruzuku kutoka serikali kwasababu ya uzembe.

" Tumejiridhisha kuwa uwezo wa Mkurugenzi kuiongoza Halmashauri yetu kama Mkurugenzi Mtendaji ni mdogo hivyo hafai anadidimiza maendeleo ya Halmashauri ya meru" alisema Njau. Na kuongeza.

"Tumeamua kuiomba mamlaka yake na Uteuzi ichukue hatua stahiki za kumuwajibisha ili kunusuru maendeleo ya Halmashauri ya meru"

Vilevile alisema kuwa Mkurugenzi huyo amekuwa akidharau maagizo yanayotolewa na kamati mbalimbali za baraza hilo na Kushindwa kuzitekeleza ambapo ni kuvunja kanuni na taratibu za Halmashauri.

Hata hivyo alisema kitendo cha mkurugenzi kukata posho zamadiwani ni kinyume na utaratibu kwani ziliwekwa kisheria ambapo alisema Kama kuna tatizo la kukatwa posho ni lazima sheria hiyo ingebadilishwa kwanza.


" Mwenye dhamana ya kutangaza kuwa posho zinabadilika ni Waziri mwenye dhamana hiyo lakini siyo mkuu wa mkoa, Wilaya au Mkurugenzi" alisema .


Naye Diwani wa Kikatiti Elisa Mungure ambaye ni Mwenyekiti wa madiwani alisema Mkurugenzi huyo amekuwa akiendesha Halmashauri kisiasa jambo ambalo halifai.

" Ninasikitishwa na uongo unaoelezwa na Mkurugenzi ambaye kateuliwa na mheshimiwa Rais hii ni ajabu haiwezekani kuendelea kumuamini mtu wa aina hii" alisema Mungure.


Alisema Mkurugenzi huyo amekuwa akiwqhamisha watendaji wa kata bila kufuata taratibu huku akishinikiza ofisi ya kata ya Kikatiti kuwa ni ya CCM huku ikiwa ni ofisi ya wananchi wala siyo ya chama chochote.


Kwa upande wake mkurugenzi Huyo Christopher Kazer alisema anafuata maagizo ya mkuu wa nchi na hawezi kuwanyima watu kufikiri wanavyofikiri.


" Maelekezo ya kupunguza matumizi yasiyolazima kutoka kwa mkuu wa nchi ninayafuata pia ndio maana nimepunguza matumizi mengi" alisema.


Alisema hawezi kuzuia maamuzi yanayotolewa na baraza hilo maana kwa namna moja au nyingine wamekaa wakatengeneza maamuzi hivyo hawezi kuwalazimisha kutofanya maamuzi.

Aidha pia alibainisha kuwa anaamini kabisa madiwani hawa wanataka halmashauri iendeshe kisiasa wanataka iendeshwe kama wao wanavyotaka kitu ambacho hatakubali kwani sio hakutumwa kufanya kazi ya siasa bali alitumwa kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi na serikali kwa ujumla 

Alisema kuwa anaamini haya yote yanatokea kutokana na madiwani hawa kukatwa fedha za posho na usafiri ambao walikuwa wamejiwekea bila kufuata taratibu

"ivi jamani ndugu waandishi mtu anatoka apo usa anataka alipwe nauli elfu 80 ni haki kweli wengine wanatoka apa apa wakija kikao kikichelewa kuisha wanataka walipwe fedha za kulala laki laki sasa mimi hayo yote tumeyatoa sasa ivi wanalipwa elfu 40 tu na mshahara wao upo pale pale sasa wao ndio maana wananipiga zwegwe mimi nasema nitasimamia ilani ya chama ambacho kinaongoza serikali pia nitafata sera ya muheshimiwa Rais ya kubana matumizi sitakubali wafanye vitu ovyo na ninyamaze walifikia atua wakataka hata kunigombanisha na watendaji wangu ila mimi nimeajiriwa na serikali mimi sio mwanasiasa na nitafanya kazi kama nilivyoaaidi siku nilioapishwa "alisema mkurugenzi Kazer 












Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...