Skip to main content

WAMILIKI WA BLOG TANZANIA KUKUTANA WIKI HII, NMB YADHAMINI MKUTANO HUO



Chama cha Wamiliki/Waendeshaji mitandao ya kijamii nchini (Tanzania Bloggrs Network-TBN) mapema leo Disemba, 2 imekabidhiwa cheki maalum ya kiasi cha Tsh. Milioni 10, fedha zilizotolewa na benki ya NMB kama wadhamini wakuu wa Mkusanyiko wa ‘Bloggers’ kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Katika tukio hilo, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Bwana Joachim Mushi amepongeza benki ya NMB kwa kuweza kudhamini tukio hilo muhimu na la kihistoria kwani litasaidia wana blogger kwa ujumla kuweza kukutana pamoja na kujifunza kile ambacho wanapaswa kuwahabarisha Umma kupitia blog zao.

“Tunawapongeza benki ya NMB kwa udhamini huu na tunawaomba sana waendelee kutudhamini kwani kazi iliyopo mbele yetu kwa sasa ni kutoa elimu sahihi kwa wenzetu ambao watajumuika katika mkutano huu utakaofanyika siku mbili yaani 5 na 6 Desemba,2016. Kwa washiriki takribani 150 kutoka Tanzania nzima ambapo pia tukio hilo litafuatiwa na mkutano mkuu kwa wanachama hai wa TBN na kujadili mambo mbalimbali,” alieleza Joachim Mushi.

Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania Bloggers Network-TBN kwani inaamini kufanya hivyo ni moja ya njia ya kufikisha ujumbe kwa jamii hasa kupitia mitandao ya kijamii.

“NMB imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na wadau wa habari mbalimbali na sasa tunashirikiana na TBN na tumeweza kutoa kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka utakaofanyika 5 na 6 Desemba mwaka huuna. Pia kama munavyofahamu kuwa NMB ipo karibu yako hivyo kupitia mitandao ya kijamii na Blog itaendelea kufikisha habari zetu kwa jamii kwa wigo mpana zaidi.” alieleza Ofisa Uhusiano huyo, Doris Kilale.

Mkutano huo unatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam hiyo 5 na 6 Desemba katika ukumbi wa wa mikutano wa makao makuu ya jengo la Golden Jubilee PSPF.

Aidha, mbali na Benki ya NMB kuwa wadhamini wakuu katika tukio hilo, pia wadhamini wengine ni pamoja na NHIF,SBL, PSPF na Coca Cola ambao wote kwa pamoja wamejitokeza kufanikisha katika tukio hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...