Skip to main content

CHAWABATA CHAPINGA MANISPAA YA ILALA KUKAGUA LESENI ZA WAUZA VILEO USIKU





Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akipinga zoezi linalofanywa na Manispaa ya Ilala la kukagua leseni za wauza vileo usiku. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.


Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck akitoa ufafanuzi katika mkutano huo.




Na Dotto Mwaibale


CHAMA cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata) kimepinga zoezi linalofanywa na Manispaa ya Ilala la kukagua leseni za wauza vileo usiku.


Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa chama hicho, Ali Hussein alisema zoezi hilo linawatisha wateja wanapokuwa wakipata vinywaji katika baa mbalimbali.


Hussein alisema chama hicho kimepokea malalamiko kutoka kwa wamiliki wa baa ambao ni wanachama wao.


Alisema wiki moja kabla ya kuanza kwa sikukuu za mwishoni mwaka maofisa biashara wa Manispaa ya Ilala walikuwa wakipita katika baa mbalimbali maeneo ya Ukonga na vitongoji vyake kuanzia saa mbili usiku kukagua leseni.


Alisema maofisa hao walikuwa wameongoza na askari polisi waliokuwa na bunduki jambo ambalo kiusalama sio zuri.


"Huu utaratibu wa kukagua leseni usiku na mtutu wa bunduki unaweza kutoa fursa kwa wahalifu nao kwenda kwenye mabaa na kujifanya ni maofisa biashara na kufanya uporaji tunaomba serikali kuliangalia jambo hili" alisema Hussein.


Alisema hali hiyo imejitokeza baada ya serikali kuzuia baa kufunguliwa asubuhi kama ilivyokuwa awali ambapo chama hicho oktoba mwaka jana kiliiomba serikali kupitia mtandao huu na katika vyombo vya habari kuruhusu kufunguliwa kwa baa wakati wote ili kutoa nafasi ya wauza vileo kufanya biashara na kuweza kukusanya fedha za kulipa kodi ya serikali.


Alisema kwa nyakati za mchana ni vigumu kukuta baa zikiwa wazi na ndio maana maofisa hao wameamua kwenda usiku kukagua leseni hizo jambo ambalo ni hatari kwa wateja na maofisa hao


"Muda wa kufungua baa kuanzia saa 10 jioni unawaathiri wateja wetu kwani kwa masaa matano ya kufanyabiashara ya vileo na vinywaji vingine ni mchache mno" alisema Hussein.


Alisema hatua hiyo ya serikali ya kuamuru baa kufunguliwa kuanzia saa 10 imeathiri wahudumu wa baa ambao wengi wao wamepunguzwa kazi ambapo wanaiomba serikali kuangalia jambo hilo.


Meneja wa Baa ya Serengeti iliyopo eneo la mabaa Banana katika manispaa hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Emanuel alisema kitendo cha maofisa hao kukagua leseni za biashara usiku ni kigeni kwao na kinawatisha wateja wao ambapo ameomba manispaa kuangalia upya muda wa kufanya ukaguzi huo.


Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Neema Njau alisema zoezi hilo lipo kisheria na linafanywa na kamati maalumu iliundwa na manispaa hiyo ambayo ipo chini ya wakuu wa polisi wa wilaya hiyo.


"Ukaguzi wa leseni hizo hauwezi kufanyika mchana kwa kuwa baa nyingi zinakuwa zimefungwa lakini wasiliana na ofisa biashara wa manispaa atakupa maelezo mazuri zaidi" alisema Njau. 

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...