Skip to main content

CHUO CHA AFRICA GRADUATE UNIVERSITY CHAWATUNUKU PhD WANAOFANYA KAZI ZA JAMII NCHINI




Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University cha jijini Dar es Salaam, Profesa Stiven Nzowa, akiongoza mahafali ya kuwatunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) wanaharakati na watumishi wa mungu nane pamoja na wengine kadhaa waliotunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili HDD Dar es Salaam jana. 




Mwanaharakati wa Haki za Watoto ambaye ni Rais wa Tanzania Music Foundation Dk.Donald Kisanga aliyetunukiwa PhD ya masuala ya Usimamizi na Uongozi wa Biashara akiwa kwenye mahafali ya 30 ya Chuo cha Africa Graduate University yaliyofanyika Dar es Salaam jana.



Askofu Dk. Godfrey Mallasy wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches, akielezea kazi mbalimbali alizofanya kabla ya kutunukiwa tuzo hiyo.



Waliotunukiwa tuzo wakiwa na furaha katika picha ya pamoja.



Wageni waalikwa wakiwa na Mama Askofu Dk.Godfrey Mallasy, Debora Mallasy (mwenye kofia), alikuwepo kushuhudia mume wake akitunukiwa tuzo hiyo.



Meneja Programu na mshereheshaji katika mahafali hayo, 


Lucy Wilson akiwa kazini.



Watunukiwa tuzo hao wakiingia ukumbuni.



Wimbo wa Taifa ukiimbwa.Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Stiven Nzowa na kulia ni mke wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe.






Mama Askofu Dk.Godfrey Mallasy, Debora Mallasy akiomba kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.



Mkaguzi wa Polisi (ASP) Ezekiel Kyogo akionesha moja ya kitabu alichokiandika chenye manufaa kwa jamii. Kyogo alitunukiwa PhD.



Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha Margaret Mutaleba, akieleza kazi alizozifanya katika jamii.



Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.



Wasanii wa Bendi ya Jordan wakitumbuiza katika mahafali hayo.



Mwanahabari Tumaini Msowoya, akieleza kazi alizoziandika ambapo zimekifanya chuo hicho kumtunuku Tuzo hiyo ya Heshima.



Watoa huduma katika mahafali hayo, wakiwa katika picha ya [pamoja na Meneja Programu, Lucy Wilson.






Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Askofu Dk. Godfrey Mallasy katika mahafali hayo.



Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha, Margaret Mutaleba.



Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Godwin Maimu.



Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Donald Kisanga.



Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Mwanahabari Tumaini Msowoya.



Furaha na tabasamu baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.



Watunukiwa tuzo hizo, Dk.Donald Kisanga (kushoto) na Mkaguzi wa Polisi (ASP), Ezekiel Kyogo (kulia), wakiwa na jamaa zao baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.



Viongozi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Dk.Godwin Maimu (kushoto) na Dk.Donald Kisanga wakiwa katika picha ya pamoja.






Na Dotto Mwaibale






CHUO cha Africa Graduate University cha jijini Dar es Salaam kimewatunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) wanaharakati na watumishi wa mungu nane pamoja na wengine kadhaa waliotunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili HDD.






Watumishi waliotunukiwa tuzo hizo za heshima ni wale waliotoa mchango mkubwa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujitolea za kijamii na zikaleta manufaa kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.






Akizungumza katika mahafali ya 30 ya chuo hicho chenye makao makuu yake Sierra Leone, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Stiven Nzowa alisema kila mwaka chuo hicho kimekuwa kikitoa Tuzo za heshima na Shahada za Uzamili kwa watanzania waliotoa mchango wa kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali.






"Tunao watunuku tuzo hizi tuzo za heshima ni watu waliokuwa na umri wa miaka 60 ambao wanafanya kazi za kijamii katika nyumba za ibada kwa zaidi ya miaka 15 na kuendelea na wale ambao umri wao ni miaka 40 hadi zaidi na wenye shahada" alisema Profesa Nzowa.






Wakizungumzia kazi walizozifanya katika jamii Askofu Dk. Godfrey Mallasy wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches alisema amefanyakazi nyingi za kijamii ikiwemo kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima na kubwa zaidi kwa kipindi cha miaka 20 amekuwa akifanya mkesha mkubwa wa kuliombea taifa amani na yeye akiwa ni mhasisi.






"Kazi hii ya kuliombea taifa amani tulianza mwaka 1997 na tumeweza kupeleka huduma hiyo hadi Zanzibar ambako kumefanyika maombi hayo kwa miaka saba na kuifanya Tanzania kuwa na amani" alisema Dk. Mallasy.






Mwanaharakati wa Haki za Watoto ambaye ni Rais wa Tanzania Music Foundation Dk.Donald Kisanga aliyetunukiwa PhD ya masuala ya Usimamizi na Uongozi wa Biashara alisema amefanya kazi nyingi za kijamii ikiwa pamoja na kuishawishi serikali kukagua fedha zinazotolewa na wahisani kwenye taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na kuwatunza watoto yatima baada ya kubaini baadhi yake zimekuwa zikifuja fedha bila ya kuwasaidia walengwa.






Mwingine aliyetunukiwa tuzo hiyo ya heshima ni Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha Margaret Mutaleba ambaye pamoja na kufanya shughuli nyingi za kijamii pia ndiye aliyemshauri Rais Dk. John Magufuli kuhusu mpango wa kufanya usafi ambao unaendelea kutekelezwa nchini kote.






Mbali na watu hao kutunukiwa tuzo hiyo ya heshima yupo mwanahabari mahiri wa gazeti la Mwananchi, Tumaini Msowoya ambaye ametunukiwa PhD kutokana na kufanya kazi mbalimbali za kijamii kupitia kalamu yake ambazo zimeleta mrejesho mkubwa kwa walengwa na kuweza kusaidiwa.






Waliotunukiwa tuzo ya heshima ya udaktari ni Donald Kisanga, Mlute Nyasa, John Pallangyo, Wilson Nyiti na Godwin Maimu.






Wengine ni Askofu Dk. Godfrey Mallasy, Ofisa wa Jeshi la Polisi Ezekiel Kyogo, Mtakwimu Margaret Mutaleba na Mwanahabari Tumaini Msowoya.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...