Skip to main content

HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI YAINGIA KATIKA TUHUMA NZITO YA ARIDHI...




MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashari kwa ajili ya kumtambulisha kuwa kiwanja ni chake sasa hivi kiwancha hicho kinataka kunyang’anywa na halmashauri ya Wilaya ya Monduli







wananchi wakiwa wamesimama na mabango yaonayoonyesha unyanyasaji wanao fanyiwa na halmashauri hiyo 








wamama wa kijiji cha Lendikinya wakiwa wamekaa kwa huzuni katika mkutano wa hadhara 















MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya


















Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo 



Habari picha na Woinde Shizza, Arusha


Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Monduli wameitupia lawama halmashauri ya wilaya hiyo na kusema kuwa inachochea migogoro ya ardhi na kuwanyima baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika vijiji vyao.


Hayo wamesema jana wakati walipokuwa wakifanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya kilichopo ndaniya halmashauri ya Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao unaongozwa na chadema kwani katika kipindi kilichopita walikuwa hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao ambayo walikuwa wanaishi tangu enzi za mababu zao .




Mmoja wawananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Songoyo Ole Matata alisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo hayo ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi wote bali uongozi huo unafukuza wananchi kulingana na chama ambacho anatokea.

“Tumekuja apa siku nyingi lakini tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri hii ichukuliwe na chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa sisi tunaotoka na tunajilikana ni wanachama wa chama cha mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu hata sisi tunaolalamika ambao tumeambiwa tumevamia msitu ni wanachama waCCM hamna mwanachama hata mmoja wa CHADEMA ambaye amefatwa akaambiwa amevamia msitu, mimi mwenyewe pembeni yangu nimepakana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo hay o hayo kunashamba la Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu waondoke ila sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu kwakweli hii sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana tunanyanyaswa sana”alisema Amina Longitoti


Akiogea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama chao hakitakaa kimya kwa hilo.


Alisema vijana wa kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi hivyo anashangazwa na kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria.

Alisema CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi na hatakuwa tayari kuona wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya mtu binafsi .


“mimi nilipata shamba hilo kama mwananchi wa kijiji hicho na sikuchukuwa shamba hilo kama kiongozi wa CCM hivyo nashangaa sana kwa kitendo cha kuingiza chama katika mambo yangu binafsi kimenisikitisha sana na kwakweli sita vumilia kabisa na kingine kinachonishangaza sio mimi tu au sisi tu ndio tunamashamba au tunamiliki ardhi katika kijiji hichi kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hili pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema lakini nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni sisi tu “alisema Sanare

Kwa upande mwananchi mungine aliyejitambulisha kwa jina la Olais Taiyai alisema kuwa ubaguzi na uchochezi uliopo ndani ya halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na hautavumilika hata kidogo kwani sio jambo jema linalofanywa na viongozi hao na kuomba serikali kuingilia kati swala hili kwani wananchi hao wanateseka na hawana pa kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa katika viwanja vyao 

Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani huo ni upepo mchafu unaovuma kupitia 

Hivi karibuni Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Monduli, lilipitisha azimio la kuchukua ardhi ya kijiji hicho kwa madai kuwa waliochukua ardhi hiyo hawakufuata sheria, akiwemo mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...