Skip to main content

MKOA WA IRINGA ASILIMIA 18 HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA








Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Eng. Stella Manyanya akisalimiana na wanafunzi wa shule za msingi za Mwaya na Tumaini zilizopo kata ya Nyalumbu wilayani Kilolo, mkoani Iringa wakati ya ziara ya ufuatilialiaji wa vituo vya elimu nje ya mfumo rasmi, vituo sitiri na elimu ya watu wazima juzi. (Picha na Friday Simbaya)





NAIBU wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Eng. Stella Manyanya amesikitishwa na kiwango cha hali ya kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu (illiteracy rate) katika Mkoa wa Iringa, ambayo ni asilimia 18.

Mkoa wa Iringa una jumla ya watu 941,238 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Eng. Manyanya aliyasema hayo juzi wakati ya ziara yake ya ufuatilialiaji wa vituo vya elimu nje ya mfumo rasmi, vituo sitiri na elimu ya watu wazima, mkoani Iringa.

Alisema kuwa takwimu hizo za kuongezeka watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu zinahitaji juhudi za serikali ili kufikia malengo ya kimataifa.

Alisema kuwa anatamani kuona katika sensa ya watu na makazi inayokuja fungu la watu wasiojua kusoma na kuandika mkoani Iringa na kwa nchi nzima linapungua.

Wakati wa ziara hiyo eng. Manyanya litembelea shule za msingi za mwaya, tumaini, ikuvala, mtua, kilalakidewa na ibumu zote za wilaya ya kilolo, mkoani Iringa.

Akiongea na wananchi wa kijiji cha kilalakidewa kata ya ibumu kitongoji cha vigulu, katika mkutano wa hadhara, naibu waziri wa elimu aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanaandikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule ili kupunguza tatizo la watu wasiojua kusoma na kuandika.

Awali, mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalla akitoa taarifa ya wilaya yake kwa naibu waziri wa elimu, alisema kuwa wilaya ina jumla ya watu wazima 10,373 wakiwemo wanaume 3,892 na wanawake 6,482 ambao hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Alisema kuwa taarifa hiyo ni kwa mujibu wa takimwu zilizokusanywa na idara ya elimu katika kipindi cha mwaka 2016 mwezi Oktoba.

Mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa atahakikisha wilaya yake inatekeleza jukumu la kutoa elimu kwa watu wote na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata fursa ya elimu.

Wilaya ya kilolo ina jumla ya vituo tisa (9)vya mpango wa elimu ya msingi kwa walioikosa (MEMKWA) vyenye jumla ya wanafuzi 198 kati yao wavulana 121 na wasichana 77.

Kwa upande wake, kaimu afisa elimu wa mkoa wa iringa, Richard Mfugale kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa, asilimia kuwa mkoa wa unaendesha program za elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.

Alisema kuwa mkoa una jumla ya vituo vya MEMKWA 18 vyenye jumla ya wafunzi 338 kati ya hao wavulana 205 na wasichana ni 133.

Mfugale alisema kuwa utoaji wa elimu ya watu wazima unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wake.

Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni honoraria kwa wawezeshaji wa program na kusababisha wawezeshaji kuacha na kutafuta shughuli zingine.

Changamoto zingine ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na uhaba wa rasilimali fedha kwa ajili ya ufuatiliaji wa program hiyo ya MEMKWA.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti ya ufuatiliaji wa program hiyo katika kitengo cha elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.

Wakati huohuo, naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Eng. Stella Manyanya amesikitishwa na hali ya miundombinu ya madarasa ya wanafunzi wa MEMKWA katika baadhi ya shule za msingi wilayani Kilolo, mkoani Iringa isiyoridhisha.

Aidha, Eng. Manyanya alitoa rai kwa wakuu wa shule nchini wanatakiwa kuwa na madarasa ya MEMKWA katika shule zao na kuagiza kuachana na walimu wa kujitolea wanaofundisha madarasa hayo.

Alisema kuwa baadhi ya shule zina walimu wakutosha hivyo watumie rasilimali watu zilizopo kufundisha madarasa ya MEMKWA ili kupunguza ubaguzi kwa wanafunzi wa MEMKWA kwa kuwaita wanafunzi wa elimu nje ya mfumo rasmi, bali waitwe wanafunzi.

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...